Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Jolt ya FurahaMfano

A Jolt of Joy

SIKU 1 YA 31

Umewahi jiuliza ni kwa nini wewe haujakuwa na uwezo wa kupata miujiza, timizo na Furaha kamilifu ambayo Biblia inazungumzia? Labda sikitisho lako linatokana na kuwa umekuwa ukitafuta Furaha katika sehemu zisizofaa. Ikiwa unaamini kwamba hayo masomo ya chuo kikuu, makazi yasio na doa au watoto watano walio na tabia nzuri ndio funguo la ufalme wa furaha... basi umekosea. Kama unadhani kupoteza paundi 27.5 au kuoa mtu wa ndoto zako au kuwa mmiliki wa pasipoti iliyojaa mihuri ya kuvutia ya kigeni itakupa pesa na kukuhakikishia furaha kamili... basi tena rafiki yangu ... umekosea. Furaha inapatikana katika sehemu moja tu ... "Katika uwepo Wake kuna Furaha kamilifu!"





Kama unataka furaha iliyoenea hadi inashinda kila hali maishani basi lazima utumie muda wako katika uwepo wa Bwana. Kama unahitaji Furaha ambayo itapinga huzuni za maisha yako yote basi lazima uchague kuwa katika uwepo Wake.





Utafanyaje hayo? Sio vigumu vile. Chagua kusoma Biblia kila siku na iwe kipaumbele... unaweza weka CD ya kuabudu na uimbe kwa pamoja! Kama wewe ni jasiri na mwenye kukata tamaa... utachagua kuinua mikono yako juu kama kitendo cha kujisalimisha unapoabudu. Chaguo lingine la kusisimua ni kutumia wakati ukiwa peke yako katika maombi kila siku. Wewe tu na Yesu. Funga mlango wa chumba chako cha kulala, piga magoti kando ya kitanda chako na uwe na mazungumzo ya moyo kwa moyo na yule ambaye anakujua zaidi na kukupenda sana.





Utakaposimama na kutoka nje ya chumba chako cha kulala ili upate kuona dunia unakoishi ... utapata ya kwamba haupo peke yako. Unaye Rafiki mzuri mpya ambaye atatembea nawe siku yote. Jina la huyu BFF wako ni nani? Unaweza muita huyu rafiki ... Furahan!

Andiko

siku 2

Kuhusu Mpango huu

A Jolt of Joy

Biblia inatuambia kwamba "Katika uwepo wake kuna furaha tele" na kuwa "furaha ya Bwana ni nguvu yetu". Furaha sio hisia tu bali ni tunda la Roho na mojawapo ya silaha bora katika gala letu la kupigana na kuvunjika moyo, ...

More

Tungependa kushukuru Carol McLeodkwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.justjoyministries.com

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha