Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Jolt ya FurahaMfano

A Jolt of Joy

SIKU 5 YA 31

Paulo na Sila walipigwa mpaka wakachubuliwa na kuvuja damu. Mavazi yao yalichanika na walichokuwa wanahitaji ni matibabu tu. Paulo na Sila, watu hawa wakuu wa Mungu waliokuwa wakisafiri katika ulimwengu wa wakati huo wakitangaza injili ya Yesu Kristo, walitupwa katika gereza huko Rumi na miguu yao kufungwa na minyororo.



Gereza la Rumi ilikuwa ni mahali ambapo wangepata ugonjwa wa kichaa, iliwachukua usiku chache katika hili gereza, mahali ambapo ungeweza kupoteza ufahamu. Waliketi chini sakafuni, palipo jaa mikojo na matapishi. Wafungwa walipata mlo mmoja tuu kwa siku ambao ulijumuisha mkate vuguvugu, uliokaribu na kuharibika, maji machafu ambayo tayari yametumika na vitu vingi vibaya ambavyo havisemeki.



Kila mara mlinzi alileta chakula, na kuhakikisha anampiga teke mfungwa sehemu ambayo itamletea maumivu makali. Wafungwa wa Kirumi walikuwa wakiketi kwenye vinyesi vyao wenyewe siku hata siku. Na kulikuwa na wadudu wasumbufu waliokuwa wakiwatambaa kwenye miili yao. Buibui walikuwa wakiingia na kutoka puani mwa wafungwa na panya wakizunguka hovyo sehemu zao za siri kwa kuwa wafungwa walikuwa hawana mavazi.



Usiku wa manane, wakati watu wengi wamekata tamaa na kukosa tumaini, Paulo na Sila walipata furaha! Waliigundua katika hali ya kunuka kwa gereza katika giza la kukataa tamaa. Waliigundua amani kwa miguu yao iliyofungwa na katika uchafu wao wenyewe.



Paulo na Sila walichagua kumwabudu Yesu katika wakati mgumu sana katika maisha yao. Paulo na Sila walipata furaha!... sasa ... wewe una udhuru gani?!



Kama wakristo, tunao wajibu... ndiyo... wajibu wa kiungu... kukutana na madhila ambayo tunaweza kupata kwa furaha ya kudharau!



Unapoamua kuingia katika sifa bila kizuizi usiku wa manane katika maisha yako, kuwa macho! Mbingu zinaweza kuanza kutikisa misingi ya maisha yako ili kukuweka huru mbali na mazingira yanayokupofusha.
siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

A Jolt of Joy

Biblia inatuambia kwamba "Katika uwepo wake kuna furaha tele" na kuwa "furaha ya Bwana ni nguvu yetu". Furaha sio hisia tu bali ni tunda la Roho na mojawapo ya silaha bora katika gala letu la kupigana na kuvunjika moyo, ...

More

Tungependa kushukuru Carol McLeodkwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.justjoyministries.com

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha