Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Jolt ya FurahaMfano

A Jolt of Joy

SIKU 6 YA 31

Unapokuwa na furaha maishani mwako, itaongeza ushuhuda wako! Furaha inaporejeshwa katika maisha yako, utakuwa na uwezo wa kuleta mabadiliko katika siku za kuenenda kwako hapa duniani. Wenye dhambi watakusikia kwa sababu una furaha. Watenda maovu watapenda kusikia kile unachokisema utakapoonesha furaha ambayo inapatikana katika wokovu.



Je, si ndivyo tunapenda? Wote tunapenda kuleta mabadiliko tukiwa hai hapa duniani. Tunataka tuache alama ya maisha yetu tukiwa duniani. Tunataka maisha yetu yawe na faida zaidi ya maneno yaliyoandikwa kwenye kaburi. Tunataka kuacha urithi wa maisha yetu kwa wale ambao tulikutana nao katika maisha. Furaha itakuwezesha kuleta hayo mabadiliko kwa mtu mwingine.



Furaha itatia nguvu ushuhuda wako na utakuwa na uwezo wa kubadilisha maisha ya mtu mwingine. Kama ulidhani furaha ilikuwepo ili ujisikie vizuri unahitaji kubadilisha mawazo yako! Mungu anataka kizazi chenye kujawa na furaha na watu walio tayari kuleta athari katika ulimwengu tunaoishi. Mimi nimo... wewe je?!
siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

A Jolt of Joy

Biblia inatuambia kwamba "Katika uwepo wake kuna furaha tele" na kuwa "furaha ya Bwana ni nguvu yetu". Furaha sio hisia tu bali ni tunda la Roho na mojawapo ya silaha bora katika gala letu la kupigana na kuvunjika moyo, ...

More

Tungependa kushukuru Carol McLeodkwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.justjoyministries.com

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha