Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 16

16
Wimbo wa Imani na Usalama kwa Mungu
Wimbo wa Daudi.
1 # Zab 25:20 Mungu, unihifadhi mimi,
Kwa maana nakukimbilia Wewe.
2Nimemwambia BWANA, Ndiwe BWANA wangu;
Sina wema ila utokao kwako.
3Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora,
Hao ndio niliopendezwa nao.
4Huzuni zao zitaongezeka
Wambadilio Mungu kwa mwingine;
Sitazimimina sadaka zao za damu,
Wala kuyataja majina yao midomoni mwangu.
5BWANA ndiye fungu la posho langu,
Na la kikombe changu;
Wewe unaishika kura yangu.
6Kamba zangu zimeniangukia mahali pema,
Naam, nimepata urithi mzuri.
7Nitamhimidi BWANA aliyenipa shauri,
Naam, mtima wangu umenifundisha usiku.
8 # Mdo 2:25-28 Nimemweka BWANA mbele yangu daima,
Kwa kuwa yuko kuumeni kwangu, sitaondoshwa.
9Kwa hiyo moyo wangu unafurahi,
Nao utukufu wangu unashangilia,
Naam, mwili wangu nao utakaa kwa kutumaini.
10 # Mdo 13:35; Zab 49:15; Mdo 2:27; Dan 9:24; Lk 1:35 Maana hutakuachia kuzimu nafsi yangu,
Wala hutamtoa mtakatifu wako aone uharibifu.
11 # Mdo 2:28 Utanijulisha njia ya uzima;
Mbele za uso wako ziko furaha tele;
Na katika mkono wako wa kuume
Mna mema ya milele.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 16: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha