Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Jolt ya FurahaMfano

A Jolt of Joy

SIKU 8 YA 31

Mimi si daktari, lakini nina orodha ya madawa kwa ajili yako!



Kama unapigana na msongo wa mawazo au huzuni, mara tatu kutwa weka muziki wa nyimbo za kusifu na kuabudu. Utataka kuinua mikono yako juu kwa kumwabudu au kaa kimya na utulie katika uwepo wake. Kwa moyo wa ujanja, naomba nikutie moyo kuungana na Daudi kucheza mbele za Bwana! Chukua dakika 5-10 kila asubuhi, mchana na usiku fuatisha wimbo na kuabudu.

Kama tiba moja haikutoshi, jaribu hii: mara tatu kutwa fungua Biblia yako na usome mstari mmoja ama miwili. Kama uko katika huzuni, anza mwanzo wa kitabu cha Zaburi na usome mstari wa 3-5 mara moja. Acha maneno ya mtunga zaburi yazame moyoni mwako na yalete nguvu ya uponyaji maishani mwako.



Mara tatu , tumia muda mchache katika maombi, ukimwombea mtu mwingine. Tunza utaratibu wa kuandika maombi ya watu. Unapojitoa kwa ajili ya kuwaombeabwengine, baraka na nguvu zinakurudia wewe katika maisha yako.



Mwishowe, mara moja kwa juma tenga muda wa kumhudumia mtu. Kaa na mtoto wa mama ali apate muda wa kupumzika. Mpekele mama mjane kwenye mgahawa na usikilize anachokipitia. Jitolee kutenegeneza chakula kwa mtu ambaye hajisikii vizuri. Usidharau nguvu ya ukarimu. Ukarimu ni pacha wa furaha... huwezi kuwa na mmoja pasipo mwingine!
siku 7siku 9

Kuhusu Mpango huu

A Jolt of Joy

Biblia inatuambia kwamba "Katika uwepo wake kuna furaha tele" na kuwa "furaha ya Bwana ni nguvu yetu". Furaha sio hisia tu bali ni tunda la Roho na mojawapo ya silaha bora katika gala letu la kupigana na kuvunjika moyo, ...

More

Tungependa kushukuru Carol McLeodkwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.justjoyministries.com

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha