Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Jolt ya FurahaMfano

A Jolt of Joy

SIKU 7 YA 31

Furaha siyo kitu cha kawaida katika maisha bali ni mwitikio wa kitofauti katika maisha. Na ndiyo maana ni tunda la roho na haitokani na wewe. Furaha siyo jambo linalotokea tuu kwenye mazingira yako ila ni muujiza unaotokea nyakati za giza za ulimwengu huu unaokufa uwepo wa Mungu unapodhihirika katika maisha yako. Furaha unayoiona na kuipata inatokana na ushirika wako na yeye.



Hukuumbwa kwa ajili ya kupata msongo wa mawazo au udhaifu wa kiroho; hukuumbwa kwa ajili ya kusengenya au kuwa na uchungu moyoni. Hukuumbwa kwa ajili ya kumnunia mume wako, kuendeleza misuguano katika kanisa au kuwafokea watoto wako. Uliumbwa kwa ajili ya furaha.



Kutatokea nini nikiamua kujaza mchanga badala ya mafuta kwenye tanki gari ili kuokoa fedha hizo za mafuta? Si kwamba sitafika huko niendako bali pia nitaliharibu gari langu! Na hii pia ni jambo la kusikitisha wakati wakristo wanataka kuendesha maisha yao katika msongo wa mawazo, uchungu au hasira. Huwezi kufika mwisho wa safari yako.



Uliumbwa ili uwe mkristo anaayezaa matunda! Hutaweza kuzaa matunda ambayo ulikusudiwa kuzaa mpaka utakapoamua kukaa na Yesu. Kila siku... siku nzima jiachie kwake na kujua kitu alichonacho kwa ajili yako. Rutubisha maisha yako na neno la Mungu, kuabudu na maombi. Kiasi kwamba Yesu anajaa moyoni mwako kiasi cha wewe kuwa na furaha tele!
siku 6siku 8

Kuhusu Mpango huu

A Jolt of Joy

Biblia inatuambia kwamba "Katika uwepo wake kuna furaha tele" na kuwa "furaha ya Bwana ni nguvu yetu". Furaha sio hisia tu bali ni tunda la Roho na mojawapo ya silaha bora katika gala letu la kupigana na kuvunjika moyo, ...

More

Tungependa kushukuru Carol McLeodkwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.justjoyministries.com

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha