Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Jolt ya FurahaMfano

A Jolt of Joy

SIKU 31 YA 31

Kuogopa, hofu au Mashaka yanaweza kutafsiriwa kwamba ni kukosa tumaini kwa Mungu anayekupenda upeo na afanyae mambo yote kuwa mema kwa ajili yako. Unapokuwa umezidiwa na hofu, unaamini kwamba matatizo yako ni makubwa kushinda hata uwezo wa Mungu. Unapojawa na hofu, unadhani kwamba dhambi zako ni nyingi hata Mungu hawezi kukusamehe. Kama unakuwa na mashaka, ni bahati mbaya na unashawishika kwamba maisha yako hayawezekani na hata Mungu hawezi kuyarekebisha tena.



Kama una hofu ya kupitiliza, hutaweza kupata furaha iliyokusudiwa kwako. Furaha na Hofu ni vitu viwili tofauti. Hofu katika hatua mbaya zaidi kama kutokuamini kuwa Mungu yupo. Ni kwa jinsi gani mtu anaweza kuishinda hofu au Mashaka?



Biblia inatuambia kwamba amani ni matokeo ya kumwamini Mungu. Je, unaweza kumwamini? Utamwamini leo? Unaweza kutangaza kwa “ Yesu, ninakuamini kwa moyo wangu wote! Naamini kwamba hakuna lisilowezekana kwako na kwamba una mipango mizuri kwa ajili ya maisha!”



Unapoijaza nafsi yako na akili yako na neno la Mungu, utakuwa huru na hofu ya mabaya. Unapomkiri Mungu kwa jinsi na kwamba anaweza kutimiza yote aliyoyakusudia maishani mwako, basi hofu na mashaka vitapotea kwa muujiza katika maisha yako. Na kitu gani kitabaki katika maisha yako ya mashaka na hofu? Utajikuta ni mtu aliyebarikiwa kwa furaha katika maisha yako!
siku 30

Kuhusu Mpango huu

A Jolt of Joy

Biblia inatuambia kwamba "Katika uwepo wake kuna furaha tele" na kuwa "furaha ya Bwana ni nguvu yetu". Furaha sio hisia tu bali ni tunda la Roho na mojawapo ya silaha bora katika gala letu la kupigana na kuvunjika moyo, ...

More

Tungependa kushukuru Carol McLeodkwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.justjoyministries.com

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha