Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Jolt ya FurahaMfano

A Jolt of Joy

SIKU 3 YA 31

Unapompokea Yesu moyoni mwako kama Bwana na Mwokozi, ulimwengu mpya wa furaha ambayo hukuwahi kuipata inafunguliwa kwako! Mungu alijua kwamba maisha hapa duniani hayatakuwa makamilifu bali tutapata adha, huzuni na kukatishwa tamaa katika siku zetu. Ili kupambana na siku hizo zenye maumivu makali, alitupa zawadi ya furaha ili ituinue juu ya matatizo yetu ya hapa duniani! Furaha ni muonjo wa mbinguni ambao umetolewa kwa wale wanaomjua Yesu kama Bwana na Mwokozi wao. Furaha ni uwezo wa kuona baraka katika uanadamu wetu ambazo Yesu anaziona katika uungu wake.



Furaha ni imara, ikionesha matunda ya uhusiano wa ndani na Mfalme wa Wafalme wote.



Unapofanya maamuzi yako ya dhati kuwa na ushirika na Yesu na kujikabidhi chini ya ubwana wake na mamlaka yake, unafanya maamuzi ya kupokea furaha katika maisha yako. Furaha haitegemei kipato chako, ubora wa mahusiano yako au anuani ya mtaa wako bali inategemeana na uchaguzi wako kwake katika magumu yote ya maisha. Unapochangua kumpa Yesu Kristo maisha yako, furaha inakuchagua wewe!

Andiko

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

A Jolt of Joy

Biblia inatuambia kwamba "Katika uwepo wake kuna furaha tele" na kuwa "furaha ya Bwana ni nguvu yetu". Furaha sio hisia tu bali ni tunda la Roho na mojawapo ya silaha bora katika gala letu la kupigana na kuvunjika moyo, ...

More

Tungependa kushukuru Carol McLeodkwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.justjoyministries.com

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha