Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Jolt ya FurahaMfano

A Jolt of Joy

SIKU 2 YA 31

Kila kitu ninachokijua kuhusu kilimo nilijifunza kutoka kwa babangu ambaye alilelewa katika shamba la familia yake siku zilizotangulia vita vya dunia vya pili. Baba alipenda sana udongo na mazao kutoka kwa udongo. Muda wake mwingi wa furaha ulitumika kwa kujichafua kwa kulima na kupanda mbegu kwenye ardhi nyakati za mvua, kutoa magugu nyakati za jua kali kisha kuvuna mazao ambayo yeye na Mungu walikuwa wamepanda!





Haya ndio nilijufunza kutoka kwa babangu: Ukipanda mbegu za tango basi utavuna tango zinazong'aa. Mbegu za tango kamwe haziwezi zalisha vitunguu au mahindi au figili. Ukipanda mahindi utavuna mahindi. Mahindi hayawezi kuzalisha maharagwe ... au maembe... au ndizi. Daima utavuna ulichokipanda. Mbegu zinaweza tu zalisha kile ambacho kanuni za maumbile zake huamua.





Huu pia ni ukweli katika ufalme wa wanyama kwa sababu paka anaweza zalisha tu kinyaunyau wala sio tembo, punda au nguruwe. Wanyama, binadamu na wadudu huzalisha tu kile ambacho kanuni za maumbile yao huamua.





Hata hivyo, katika ufalme wa Mungu, kanuni hii haitumiki kikamilifu. Katika bustani la Mungu, ukipanda kwa machozi lazima utavuna kwa furaha! Kama umelala siku nyingi kwa machozi, ukilia na umekuwa na uzoefu wa huzuni, majonzi na masikitiko ... usife moyo! Furaha ipo njiani yaja! Machozi yako yameweka mbolea kwa mbegu ya furaha ambayo Mungu amepanda katika bustani la maisha yako.





Wale ambao wamepanda machozi ya msiba, huzuni na kuvunjika moyo wana uwezo mkubwa wa Furaha!





Furaha inawezekana hata kama umekuwa na hisia za maumivu. Lakini ni jambo la uhakika katika ufalme wa Mungu. Mungu hajakusahau lakini yuko na furaha ya kushirikiana na wewe katika mchipuko wa furaha! Wakati mbaya sana wa maisha yako una uwezo wa kuzalisha matokeo bora sana.

Andiko

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

A Jolt of Joy

Biblia inatuambia kwamba "Katika uwepo wake kuna furaha tele" na kuwa "furaha ya Bwana ni nguvu yetu". Furaha sio hisia tu bali ni tunda la Roho na mojawapo ya silaha bora katika gala letu la kupigana na kuvunjika moyo, ...

More

Tungependa kushukuru Carol McLeodkwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.justjoyministries.com

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha