Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 6Mfano

Soma Biblia Kila Siku 6

SIKU 1 YA 30

Ilikuwa lazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza; lakini kwa kuwa mnalisukumia mbali ... angalieni, twawageukia Mataifa (m.46). Ni nini kilichowafanya Wayahudi wasiipokee Injili? Ni wivu: Watu wengi, karibu mji wote, wakakusanyika walisikie neno la Mungu. Bali Wayahudi, walipowaona makutano, wakajaa wivu, wakayakanusha maneno yaliyonenwa na Paulo, wakibisha na kutukana (m.44-45)! Ole wao! Je, mtumishi wa Kanisa la Bwana, unamwonea mtumishi mwenzako wivu akipata ufunuo ambao wewe hukupata? Acha wivu wako. Sikiliza ujumbe wake; usije ukakosa uzima wa milele! Wayahudi walikuwa wa kwanza! Ndivyo waumini kanisani tulivyo wa kwanza leo kuupokea uamsho wa Injili! Tusiipoteza nafasi yetu! 

Andiko

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 6

Soma Biblia Kila Siku 6 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.

Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha