Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 6Mfano

Soma Biblia Kila Siku 6

SIKU 2 YA 30

Mungu ni shujaa. Ni mwenye utukufu, enzi na mamlaka. Anastahili kusifiwa na kuogopwa kwa matendo yake makuu kwa wanadamu. Kama askari hodari amezivunja zana za vita za maadui, na kufanya maajabu mengi ya wokovu mkubwa. Rudia m.9 ukilinganisha na Mik 6:8. Mungu alisimama ili kuhukumu na kuwaokoa wapole wa dunia wote pia. ↔Bwana anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako!Zingatia kuwa ndio wapolewanaookolewa! Tena Mungu ndiye mwamuzi mwenye haki anayewalinda hao wapole wote. Kwa matendo hayo, anastahili kutegemewa na kila kiumbe kwa ajili ya mamlaka yake ya pekee mbinguni na duniani.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 6

Soma Biblia Kila Siku 6 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.

Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha