Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 6Mfano

Soma Biblia Kila Siku 6

SIKU 8 YA 30

Kwa baadhi ya Wakristo wa Kiyahudi ilikuwa ni jambo gumu sana kuelewa na kukubali kwamba Mtaifa aliweza kuwa Mkristo safi na mtoto kamili wa Mungu bila kufanywa kuwa Myahudi (ling. m.1:Wakashuka watu waliotoka Uyahudi wakawafundisha wale ndugu ya kwamba, Msipotahiriwa kama desturi ya Musa hamwezi kuokoka.Na m.5: baadhi ya madhehebu ya Mafarisayo walioamini wakasimama wakisema, Ni lazima kuwatahiri na kuwaagiza kuishika torati ya Musa). Hawakutambua sawasawa kwamba Agano Jipya alilolitengeneza Mungu kwa Yesu Kristo ni kwa ajili ya wanadamu wote, tofauti na Agano lile la kale. Siri hiyo hawakujulishwa wanadamu katika vizazi vingine; kama walivyofunuliwa mitume wake watakatifu na manabii zamani hizi katika Roho; ya kwamba Mataifa ni warithi pamoja nasi wa urithi mmoja, na wa mwili mmoja, na washiriki pamoja nasi wa ahadi yake iliyo katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili(Efe 3:5-6). Ila huu mkutano wa mitume ulithibitisha jambo hili, na Wakristo wa kimataifa walifurahi: Waliochaguliwa na mkutano wakawapa ile barua. Nao walipokwisha kuisoma wakafurahi kwa ajili ya faraja ile. (m.30-31)! Nasi tumshukuru Mungu sana kwamba neema yake hii pia imefunuliwa Tanzania!

siku 7siku 9

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 6

Soma Biblia Kila Siku 6 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.

Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha