Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 6Mfano

Soma Biblia Kila Siku 6

SIKU 7 YA 30

Maelezo ya Barnaba na mtume Paulo kuhusu Mataifa kuipokea Injili (habari za ishara na maajabu, ambayo Mungu aliyafanya kwa ujumbe wao katika Mataifa; m.12) hayakuwa tofauti na yale ya mtume Petro: Na Mungu, ajuaye mioyo ya watu, akawashuhudia, akiwapa Roho Mtakatifu vile vile kama alivyotupa sisi; wala hakufanya tofauti kati yetu sisi na wao, akiwasafisha mioyo yao kwa imani(m.8-9). Yakobo, kiongozi wa usharika mama, aliona kuwa haya pia yanapatana na maneno ya manabii wa Agano la Kale. Kwa msingi huu alitoa uamuzi wa suala hilo, kwa sababu Kanisa limejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni(Efe 2:20). Agano jipya la Kristo ni agano la neema. Twaamini kwamba tutaokoka kwa neema ya Bwana Yesu(15:11). Tazama, mimi Paulo nawaambia ninyi ya kwamba, mkitahiriwa, Kristo hatawafaidia neno. Tena namshuhudia kila mtu atahiriwaye, kwamba ni wajibu wake kuitimiza torati yote. Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema. Maana sisi kwa Roho tunalitazamia tumaini la haki kwa njia ya imani. Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo(Gal 5:2-6).

siku 6siku 8

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 6

Soma Biblia Kila Siku 6 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.

Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha