Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023

SIKU 6 YA 30

Tunafikiri Mungu ni kama sisi. Sisi tukikosewa na mtu hatuwezi kumsamehe hivi hivi tu. Lazima afanye tendo la upatanisho. Sasa sisi tumemkosea Mungu. Yeye pia anataka tendo la upatanisho lifanyike. Ila haki yake ni tofauti na haki yetu (10:3,Kwa maana, wakiwa hawaijui haki ya Mungu, na wakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu)! Maana alipoona kuwa sisi tumeshindwa kutenda tendo la upatanisho la kumridhisha akaamua mwenyewe kwa upendo wake kutenda tendo hili kwa Mwana wake! Na bila sisi kumwomba. Ni kama Mungu anavyosema katika m.20:Nalipatikana nao wasionitafuta, Nalidhihirika kwao wasioniulizia. Kumbuka pia jambo hili lilivyosisitizwa katika 5:8,Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu tulipokuwa tungali wenye dhambi! Haya si mambo ya kawaida. Kwa hiyo tunahitajikuyasikiatena na tena!

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa septemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi k...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha