Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023

SIKU 7 YA 30

Ni vivi hivi wakati huu sasa, yako mabaki waliochaguliwa kwa neema(m.5). Mtume Paulo mwenyewe (m.1) pamoja na mitume wengine ni sehemu ya mabaki haya, yaani ni Waisraeli waliomfuata Yesu na kukiri kwamba ni Kristo na Mwana wa Mungu. Ni wazi kuwa mitume hao, na hasa Paulo, hawakuwa na matendo ambayo yaliwastahilisha kuitwa na Yesu. Ni kwa neema ya Mungu tu (m.6:Ikiwa ni kwa neema, haiwi kwa matendo tena, au hapo neema isingekuwa neema. Ukipenda, linganisha na 1 Tim 1:12-17)! Haya kweli yanaonyesha kuwa Mungu hajawasukumia mbali watu wake. Paulo anaandika katika m.1 kwamba yeye mwenyewe ni uthibitisho:Mimi nami ni Mwisraeli.Lakini walio wengi Mungu aliwaadhibu, kwa sababu kile walichokitafuta hakikuwa cha Mungu.Kama ilivyoandikwa, Mungu aliwapa roho ya usingizi, macho hata wasione, na masikio hata wasisikie, hata siku hii ya leo.Na Daudi asema, Meza yao na iwe tanzi na mtego, Na kitu cha kuwakwaza, na malipo kwao;Macho yao yatiwe giza ili wasione, Ukawainamishe mgongo wao siku zote(m.8-10).

siku 6siku 8

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa septemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi k...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha