Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023

SIKU 5 YA 30

Paulo alitaka sana Wayahudi waokoke.Kwa maana nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa(m.2).Huko nyuma Paulo mwenyewe alikuwa namna iyo hiyo. Aliwaudhi Wakristo kwa sababu alikuwa na juhudi kwa ajili ya Mungu! Ila alikuwa kipofu. Hakumtumikia Mungu bali alimwudhi Mungu (unaweza kuangalia ushuhuda wake mwenyewe katika Mdo 22:3-8). Kumbe, mtu anaweza kuwa na juhudi kwa ajili ya Mungu bila kuwa mtoto wa Mungu na bila kuwa mwenye haki mbele yake. Zingatia m.3 ambapo Paulo anaandika kuhusu Wayahudi kuwawakiwa hawaijui haki ya Mungu, na wakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu.Tukubali kuokoka kwa neema. Tumkubali Yesu,kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki(m.4)!

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa septemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi k...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha