Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022

SIKU 1 YA 30

Mwandishi ni mtume Paulo. Wapokeaji wa waraka ni Wagalatia, wakazi wa Asia Ndogo, lakini sisi nasi ni wapokeaji wa Neno la Mungu. Hapa mwanzoni mwa waraka huu Paulo anawasalimu Wagalatia. Si yeye tu, lakini ni pamoja na ndugu wote walio pamoja nami. Hata mtume Paulo alihitaji ushirika wa Wakristo wengine. Ndiyo maana anawalimu akisema, Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba, na kwa Bwana wetu Yesu Kristo (m.3). Kusudi la mtume Paulo kuwasalimu Wagalatia ni kuwakumbusha kwamba wakiwa Wakristo wanazo neema na amani zitokazo kwa Mungu. Unaweza kulinganisha na Gal 6:18 anaposema, Ndugu zangu, neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja na roho zenu. Amina.

Andiko

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022

Soma Biblia Kila Siku Septemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Septemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu uliloso...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/

Mipangilio yanayo husiana

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha