Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022

SIKU 2 YA 30

Katika mistari hii ya leo twaona kusudi la mtume Paulo la kuwaandikia Wagalatia waraka huu: Waligeukia injili nyingine, iliyo kinyume cha Injili ya Mungu. Sisi Wakristo tunao wajibu wa kujaribu mafundisho tusikiayo. Ndivyo tunavyoambiwa katika 1 Yoh 4:1-3, Msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani. Katika hili mwamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu. Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani. Mtume Paulo anawalaani waliogeuza Injili ya Mungu. Hao walidai kwamba Wakristo washike sheria, na hata kutahiriwa, ili wapokelewe na Mungu. Sababu ya mtume Paulo kuwalaani waliofundisha namna hii zimeelezwa katika Gal 5:2-6 hasa anaposema,Mimi Paulo nawaambia ninyi ya kwamba, mkitahiriwa, Kristo hatawafaidia neno. Tena namshuhudia kila mtu atahiriwaye, kwamba ni wajibu wake kuitimiza torati yote. Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema. Maana sisi kwa Roho tunalitazamia tumaini la haki kwa njia ya imani. Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo!

Andiko

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022

Soma Biblia Kila Siku Septemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Septemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu uliloso...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha