Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022

SIKU 4 YA 30

Sababu ya mtume Paulo kwenda Yerusalemu tena ilikuwa kuwaeleza wakuu wa pale Injili aliyopokea - isiwe labda napiga mbio bure (m.2b). Kulikuwa na shida na ndugu za uongo. Njia nzuri kuliko zote nyingine ni kuonyesha umoja katika mafundisho. Ndivyo walivyofanya mtume Paulo na wale wenye sifa (m.6) - yaani Petro, Yohana, na Yakobo. Kwa hiyo walikubali mafundisho ya mtume Paulo. Tena m.7-9 yaonyesha kwamba walikubaliana kwamba kila mmoja anayo huduma yake. Katika mistari hii Paulo anaeleza kuwa wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza injili ya Kristo. Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe. Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe.

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022

Soma Biblia Kila Siku Septemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Septemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu uliloso...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha