Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 7Mfano

Soma Biblia Kila Siku 7

SIKU 1 YA 31

Kama sisi, pia Danieli aliona ugumu wa kuyafumbua maono katika m.8-14. Malaika anatumwa kumfafanulia. Ndiye Gabrieli ambaye pia alitangaza juu ya kuzaliwa kwa Yesu. Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti, kwa mwanamwali bikira(Lk 1:26). Maono aliyopewa Danieli, yalianza kutimia wakati alipoishi, lakini yanahusu nyakati za mwisho hasa. Wanyama wanawakilisha falme za dunia, za wakati wake. Atatokea mfalme mwenye nguvu nyingi mno, lakini ataangushwa. Maana Mungu ndiye Mkuu wa wakuu, na hakuna wa kumshinda. Zingatia ilivyoandikwa kuhusu mfalme mwenye uso mkali katika m.25: Atasimama kushindana naye aliye Mkuu wa wakuu; lakini atavunjika, bila kazi ya mikono. Uweza na haki ya Mungu vitatawala.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 7

Soma Biblia Kila Siku 7 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kuelewa zaidi.

Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha