Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 7Mfano

Soma Biblia Kila Siku 7

SIKU 9 YA 31

Kitabu cha Danieli kimejaa ujumbe uhusuo wapinzani wa Mungu. Hali ya baadaye imewekwa wazi. Uharibifu utafikia upeo wake, mfalme mfano wa mpinga Kristo atakapojitukuza mwenyewe juu ya Mungu (m.37: Hatamjali mungu awaye yote; maana atajitukuza mwenyewe juu ya wote). Hata hivyo kuna matumaini, “maana yaliyokusudiwana Mungu yatafanyika” (m.36). Waaminifu wasikate tamaa. Kuna wokovu kutoka kwa Mungu ambao haujawahi kuwepo. Wokovu huo utafuatana na ufufuo. Hapo wenye hekima ya kimungu wataonekana dhahiri waking’aa kama nyota milele na milele(12:1b-3, Wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile. Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele. Na walio na hekima watang'aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang'aa kama nyota milele na milele).

siku 8siku 10

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 7

Soma Biblia Kila Siku 7 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kuelewa zaidi.

Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha