Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 7Mfano

Soma Biblia Kila Siku 7

SIKU 2 YA 31

Haya ni maombi ya toba kwa ajili ya watu wote. Angalia Danieli alisukumwa na nini: Alisoma neno la Mungu kwa makini. Mimi Danieli, kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka(m.2). Na alimfahamu Mungu kwamba ashika maagano (m.4:Nikasema, Ee Bwana, Mungu mkuu, mwenye kutisha, ashikaye maagano na rehema kwao wampendao), kutenda haki (m.14: Bwana, Mungu wetu ni mwenye haki katika kazi zake zote azitendazo) na ana rehema nyingi (m.18:hatukutolei maombi yetu kwa sababu ya haki yetu, lakini kwa sababu ya rehema zako nyingi). Hayo huleta kujitambua kama mwenye dhambi. Hutia pia ujasiri wa kumwomba Mungu asamehe kwa ajili yake mwenyewe(m.19: Ee Bwana, usamehe; ... kwa ajili yako wewe, Ee Mungu wangu). Danieli anaanza kwa kufunga. Maombi yanahusu kuwarudisha Waisraeli nyumbani. Fuata mfano wake ukiombea kanisa lako. Tumia m.17-19 kama maombi yako:Ee Mungu wetu, yasikilize maombi ya mtumishi wako, na dua zake, ukaangazishe uso wako juu ya patakatifu pako palipo ukiwa, kwa ajili ya Bwana. Ee Mungu wangu, tega sikio lako, ukasikie; fumbua macho yako ukautazame ukiwa wetu, na mji ule ulioitwa kwa jina lako; maana hatukutolei maombi yetu kwa sababu ya haki yetu, lakini kwa sababu ya rehema zako nyingi. Ee Bwana, usikie; Ee Bwana, usamehe; Ee Bwana, usikilize, ukatende, usikawie; kwa ajili yako wewe, Ee Mungu wangu; kwa sababu mji wako na watu wako wanaitwa kwa jina lako.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 7

Soma Biblia Kila Siku 7 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kuelewa zaidi.

Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha