Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 7Mfano

Soma Biblia Kila Siku 7

SIKU 4 YA 31

Tofauti na wafalme wasiomjua Mungu waliokuwa wanaota ndoto, mtumishi wa Mungu anaona maono na kufunuliwa neno. Kwa pamoja hayo mawili humsaidia mnyenyekevu mwenye kutafuta ufahamu aelewe ujumbe wa Mungu (m.12: Akaniambia, Usiogope, Danieli; kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu, na kujinyenyekeza mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwa; nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako). Ingawa uhusiano wa Mungu na mtumishi wake ni wa upendo, kukutana na utukufu wa Mungu hufanya Danieli asibaki na nguvu. Hofu inaondolewa tu kwa kuambiwa, Usiogope. Kulikuwa na vita kali katika ulimwengu wa roho, na bado ipo, lakini hakika mapenzi ya Mungu yatafanyika (m.14: Nimekuja kukufahamisha mambo yatakayowapata watu wako katika siku za mwisho; maana maono hayo ni ya siku nyingi bado).

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 7

Soma Biblia Kila Siku 7 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kuelewa zaidi.

Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha