Maelezo ya mpango
Soma Biblia Kila Siku Mei/2022Mfano
Mkakati wa Nathani ulikamilika alipomtaka mfalme athibitishie taifa ni nani atakayetawala baada yake, baada ya kuambiwa kuna uhaini katika ufalme wake. Mfalme alimthibitishia Bath-sheba juu ya ahadi alizotoa. Na hapo hapo alitoa maagizo juu ya jinsi ya kumsimika na kumweka Sulemani katika kiti cha kifalme. Watu wote katika ufalme walisherehekea tukio hilo. Wakati wa Mungu ukifika, hakuna mashaka juu ya ukamilifu wa kusudi lake. Sulemani akawa mfalme kwa baraka zote za baba yake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Mei/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Mei pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa sik...
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/