Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Kuweka Muda Wa KupumzikaMfano

Making Time To Rest

SIKU 5 YA 5

Jaza Ili Kumwagika.



Kujawa na Roho maana yake ni hii-- asili yote ikiwa chini ya nguvu zake. Wakati nafsi imejawa na roho Mtakatifu, Mungu mwenyewe ataijaza.— Andrew Murray



Sababu ya kutaka kupumzika ni kwa sababu tumekuwa tukifanya kazi nyingi na kutumia nguvu kwa namna fulani. Na kwa sababu tumejifunza jinsi ya kupumzika na tunaweza kujisikia tumepumzika, hai maanishi tutabaki hivyo hivyo.



Tutafanya tena. 

Tutawasaidia wengine tena. 

Tutaishiwa tena kihisia. /em> 



Kupumzika kwa sababu ya kupumzika siyo tu maana halisi. Tunapumsika na kupumzika ili tuweze kufanya kazi tena. Kuna kujaa na kutiririka kwa kufanya kazi na kupumzika; ya kujaa ili tuwamwagike.



Kama tulivyokwisha kujadili, kutafakari neno la Mungu, kujitenga na kujiachanisha na vitu vinavyokuondolea matendo ya kutujaza tena. Tunapata pumziko tunapofanya haya kila siku. Kama vile miili yetu ya nyama inavyohitaji muda wa kutosha usiku ili kupona, na roho zetu zinahitaji pia. Hatuwezi kutegemea kuwa na nafsi yenye nguvu na changamfu pasipo kuwekeza kwenye katika hilo. Hatuwezi kudhani juma moja la likizo linaweza kutupeleka miezi na miezi. Lazima tuweke kila siku kwenye chombo cha mapumziko ili kuendelea. Na lazima tuwe wasikivu wakati matumizi makubwa ya akiba yamefanyika.



Katika kitabu hiki, Leading on Empty: Refilling Your Tank and Refueling Your Passion, mwandishi na mchungaji Wayne Cordeiro anatuambia kuhusu ndoto aliyopata. Mwanamke alimkabili mkulima shambani kwake na kumwomba kitu ambacho hakuwa nacho. Akamwambia "Rudi tena kesho, na nitakuwa nacho." Syule mwanamke alikasirika lakini haikumsumbua mkulima. Aliendeelea na kazi yake. Wali walikuja shambani kwake kila siku na alipokosa mayai au maziwa, aliwaambia tu "Rudini kesho nitakuwa na zaidi." Mchungaji Cordeiro alishirikiana nasi mtazamo huu alioupata baada ya kupata ndoto:



Sitaki kujifunga kwenye kufikirika, mzunguko usioisha wa kuzalisha zaidi, tengeneza zaidi au kujaribu kupita idadi ya juma lililopita. Nina muda wa kutosha kwa siku, na nataka kufanya nachoweza kufanya na moyo wangu ukihusika. Wakati muda utakapoisha, ndipo nitakaposema, "Rudi tena kesho, nitakuwa navyo zaidi.”



Tunaamka kila siku na kiwango fulani cha nguvu za akili, hisia, na kimwili. Tunapokuwa tumetoa kila kitu tunachotakiwa kutoa, lazima tupumzike. Tunapokuwa tumeishiwa, hatuwezi kufanya chochote kwa kazi yake katika maisha yetu. 



Egemea nyuma, tulia, na upumzike. Hii ni nafasi pekee na muda sahihi kujazwa upya na Roho wa Mungu. 



Tafakari




  • Unadhani unatakiwa kukutana na kila hitaji unaloliona?

  • Ni kitu gani unaweza kukiingiza kwenye siku yako ili ujisikie umejazwa

  • Andika ufunuo wowote ambao Mungu anasema na wewe kupitia masomo ya leo ya Biblia au ibada.

siku 4

Kuhusu Mpango huu

Making Time To Rest

Kupenda kazi sana na wakati wote kufanya kazi vinasifiwa sana katika ulimwengu wetu, na vinaweza kuwa ni changamoto kwa wengine. Ili kutimiza majukumu yetu na mipango yetu kwa ufanisi, lazima tujifunze kupumzika au hatut...

More

Mpango huu wa asili wa Biblia uliundwa na kutolewa na YouVersion.

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha