Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Kuweka Muda Wa KupumzikaMfano

Making Time To Rest

SIKU 3 YA 5

Sasisha/fanya upya mawazo yako kwa kujitenga.


Chochote unachokifikiria kinakuwa. Usifikirie yale unayoyapitia. Fikiria yale utakayoyafanya!— Dr. Caroline Leaf


Siku ya 2, tulijifunza jinsi ya kupumzika kwa kutafakari neno la Mungu ili matendo yetu yaendane na kweli yake. Kuna njia nyingi za kuyafanya maandiko yazame ndani ya roho zetu. Kweli yake inamwagwa kwenye mawazo yetu na tutaanza kuona vitu tofauti. Tunapotafakari neno la Mungu, mawazo yetu yatafanywa upya na tutapata pumziko ambalo hatukufikiria inawezekana.


Ili kupata zaidi katika muda wetu na neno la Mungu, tunaweza kuhusisha kujitenga kama sehemu ya maisha yetu ya kila siku. Kujitenga hakuhitaji kuwa kwa undani sana au kuwa kugumu kama ni kitu ambacho hatujakizoea kufanya. Inaweza kuwa rahisi sana kama kuandika mistari michache ya ufahamu tunayopokea wakati wa kusoma Biblia. Kuna njia nyingi za kujitenga, Tunaweza kuandika mawazo yetu au maombi yetu; watu wengine wanafanya kazi za sanaa wakati wao wa kujitenga. Hakuna njia sahihi ya kufanya hivyo. Ili kukusaidia kuanza, hapa kuna maelekezo rahisi ya kufuata:


  • Chagua mstari (au mingi) na usome. 
  • Soma tena. 
  • Andika. 
  • Muombe Mungu ufahamu na uandike.

Labda unaamua kujitenga kwa ajili ya Warumi: 8:28 ambayo inasema, “Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake."  Baada ya kusoma mara mbili au tatu, tunaandika. Tunaweza kuchagua kuandika kwa tafsiri nyingine ya Biblia. Tunamaliza muda wetu wa kujitenga kwa kumuomba Mungu ufahamu kuhusu tuliyosoma.


Tunapoleta maandiko kupitia mpango ulioelezwa hapo juu, tunaweza kuutumia kwa siku nzima. Kujitenga kila siku kunatupa muda wa kuweza kuangalia nyuma na kuona maendeleo ya kiroho tuliyofanya na njia mpya ambazo Mungu amesema nasi.


Tutaona mambo wazi wazi na kupata uelewa mpya kuhusu jinsi neno la Mungu linavyotumika katika maisha yetu na kuturejesha kutoka nje ndani. Na mawazo yetu yakiwa yamefanywa upya, tunapokea pumziko ambalo haliwezi kupatikana na starehe yoyote ya dunia.


Tafakari 


  • Umewahi kujitenga kama sehemu ya muda wako na Mungu?  
  • Chagua mstari mmoja na jitenge nao ukitumia maelekezo yalitolewa juu. 
  • Andika ufunuo ambao Mungu anasema nawe kupitia somo la leo la kusoma Biblia au ibada.
siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Making Time To Rest

Kupenda kazi sana na wakati wote kufanya kazi vinasifiwa sana katika ulimwengu wetu, na vinaweza kuwa ni changamoto kwa wengine. Ili kutimiza majukumu yetu na mipango yetu kwa ufanisi, lazima tujifunze kupumzika au hatut...

More

Mpango huu wa asili wa Biblia uliundwa na kutolewa na YouVersion.

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha