Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Kuweka Muda Wa KupumzikaMfano

Making Time To Rest

SIKU 2 YA 5

Tafakari neno la Mungu.



Kadri unavyosoma Biblia; kadri unavyolitafakari, ndivyo utakavyo shangazwa nalo.— Charles Spurgeon



Wafuasi wengi wa Kristo hawaelewi maana ya kutafakari. Tnapotafakari juu ya jambo fulani tunaweka mawazo yetu hapo. Ili kuelewa kutafakari neno la Mungu maana yake nini, hebu tusome maelezo ya Mchungaji Rick Warren. Anasema, “Inashangaza, kama unajua jinsi ya kuwa na mashaka, tayari unajua jinsi ya kutafakari juu ya neno la Mungu. Hofu ni pale unapokuwa na mawazo hasi na unawaza juu yake mara kwa mara. Unapochukua kifungu cha maandiko na kufikiria juu yake mara kwa mara, hiyo inaitwa kutafakari."



Biblia inataja kutafakari zaidi ya mara ishirini na inatutaka tutafakari neno la Mungu. Hii ni tabia yenye faida kuijumuisha katika maisha yetu ya kila siku na Mungu kama inavyoelezwa kwamba inaleta pumziko la akili na hisia kwetu na kukua kiroho.



Kadri tunavyotumia muda kusoma Biblia kila siku, tunaweza kuangalia kwa undani kifungu na kuanza mazungumzo na mungu. Ili kuelewa namna ya kutafakari mstari mmoja au miwili, hebu tugawanye waefeso 4: 31-32 inayosem, “Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya; tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi."  



Hebu tusome tena na kumwomba Mungu:



Nina uchungu? 

Ni mtu niliyekasirika? 

Maneno yangu yana ghadhabu? 

Moyo wangu una huruma? 

Nawasamehe wengine bure?
 



Ndipo tunasikiliza na kusubiri, sauti ya upole ya Mungu yenye nguvu. Mara chache sana itasikika lakini tutajua anasema nasi. Tunaweza kuruhusu tafakari hizi za maandiko kwenda nasi katika shughuli zetu za kila siku kutukumbusha juu ya uchungu wowote, hasira, matukano, ugumu wa moyo, au kutokusamehe ambavyo vinajaribu kuteka mawazo yetu.



Huku ni kutafakari neno la Mungu. 



Ukweli wa maandiko huzama ndani ya nafsi zetu tunapotafakari katika neno la Mungu.Kutafakari kunatupa kiwangi kipya cha kupumzika kwa sababu tunatumia nguvu zetu za akili kufikiria juu ya neno la Mungu na siyo kuzamisha mawazo yetu na masumbufu ya dunia. si hivyo tuu, bali tuna nguvu ya kutumia maneno haya ya kubadilisha maisha yetu kutoka kwa Mungu kuja kwetu. Hatuwezi zaidi ya kuwa vyote Mungu anavyotaka tuwe tunapofanya juhudi hiyo.



Tafakari




  • Chagua andiko kutoka katika somo la leo, au lingine utakalochagua, na litafakari. Unapolisoma, mwombe Mungu akuoneshe eneo unalomtii na unataka kufanya mabadiliko ili ukue kiroho. Ruhusu ugunduzi huu mpya ugawanye mawazo yako siku nzima.

  • Andika ufunuo ambao Mungu anazungumza na wewe kupitia somo la leo la Biblia au ibada.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Making Time To Rest

Kupenda kazi sana na wakati wote kufanya kazi vinasifiwa sana katika ulimwengu wetu, na vinaweza kuwa ni changamoto kwa wengine. Ili kutimiza majukumu yetu na mipango yetu kwa ufanisi, lazima tujifunze kupumzika au hatut...

More

Mpango huu wa asili wa Biblia uliundwa na kutolewa na YouVersion.

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha