Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Kuweka Muda Wa KupumzikaMfano

Making Time To Rest

SIKU 4 YA 5

Jitenganishe na usumbufu /p>

Kama hujitengi na mbali na ulimwengu unaokuzunguka, utavutwa na ulimwengu unaokuzunguka.— Erwin McManus



Moja ya ufafanuzi wa kumpumzika ni kuwa huru na masumbufu au kelele. Wakati huu katika maisha yetu, tunaweza kuona vitu vinavyoharibu mapumziko yetu na kutuletea wasi wasi. Vinaweza kuleta burudani kwa muda na kuonekana kama vinatuburudisha, lakini mwishowe, tunaondolewa mapumziko ya kweli.



Watu wengi sana wanaongelea njia nyingi za kujitenga na muingiliano wa ulimwengu. Kuna vitabu, makala na ujumbe unaotupa hatua tatu za kutokushughulishwa na vitu vinavyotuibia usikivu wetu. Lakini siyo kila mtu anasumbuliwa na vitu hivyo. Vinavyomsumbua mtu mmoja si sawa kwa mwingine.



Ili kujitenga na usumbufu katika maisha yetu, lazima tutafakari mambo kadhaa. Kwanza, lazima tujue kinachotusumbua. Kitu hicho kinachotuchosha kutoka kwenye vitu muhimu aidha vinaonekana ni haraka au ni mzaha wa kupoteza muda. Na cha pili, lazima tuwe tayari kuweka ajenda zetu ili watu wa muhimu katika maisha yetu wasijisikie kama kuwqasumbua.



Chochote ambacho kinaiba amani na mapumziko kwetu, lazima tuweke mipaka fulani. Yawezekana baada ya kusoma sentensi hiyo, wote tunajua kwa uhakika ni nini. Badala ya kuacha usumbufu kutuzuia kupumzika na watu muhimu katika maisha yetu, yawezekana...




  • ...hatufungui kompyuta zetu kufanya kazi wakati watoto wako macho. 

  • ...tunachagua kuangalia mambo mema badala ya kusumbuliwa na mashaka ya dunia. 

  • ..tunaweka miito maalum kwa ajili ya wana familia na wengine waende kwenye ujumbe wa sauti. 

  • ...tunachagua kutokuangalia luninga mpaka mwisho wa juma. 

  • ...kuweka pembeni mipango yetu kwa ajili ya kuishi sasa. 

  • ...tunaweka muda maalum kwa baadhi ya tovuti, App na michezo ya video.  


kama tukijikuta tuko katika muendelezo wa wasiwasi na masumbufu, lakima tupunguze au kuondoa kabisa vitu kama hivyo vinavyotufanya hivyo. Haitakuwa rahisi. Chochote ukitakacho kinahitaji kufanya kazi na kujitolea. Tusiende siku nyingine ambapo tunaruhusu masumbufu ya dunia hii yatutenge na pumziko bora la Mungu kwetu.



Tafakari




  • Jambo gani kubwa linalokusumbua kutokana na mapumziko ya kweli?

  • Unahitaji kuchukua hatua gani leo au kuzuia masumbufu katika maisha yako?

  • Andika ufunuo wowote ambao Mungu anasema nawe kupitia masomo ya leo ya Biblia au ibada.

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Making Time To Rest

Kupenda kazi sana na wakati wote kufanya kazi vinasifiwa sana katika ulimwengu wetu, na vinaweza kuwa ni changamoto kwa wengine. Ili kutimiza majukumu yetu na mipango yetu kwa ufanisi, lazima tujifunze kupumzika au hatut...

More

Mpango huu wa asili wa Biblia uliundwa na kutolewa na YouVersion.

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha