Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Waliochaguliwa: Jikumbushe Kuhusu Injili Kila SikuMfano

Chosen: Remind Yourself Of The Gospel Everyday

SIKU 6 YA 7

Katika kijiji duni ndani ya nchi ya Nepali karibu na mlima wa Evarest, takribani alsimia 80 ya wasichana watauzwa katika soko la ukahaba kwa sababu wanachukuliwa kuwa watu wa tabaka la chini zaidi katika nchi hiyo, watu wa Badi. Dini yao inafunza kwamba kwa maisha ya kale lazima walitenda dhambi nyingi zenye uzito ndio maana maisha yanawaadhibu kwa kuwatuma tena katika maisha haya katika ukoo wa Badi. Watu hata watu hawa wasaidii, kwa sababu hawataki kuyazuia maisha kuwaadhibu. Matokea yake, wasichana kutoka ukoo wa Badi ndio wanaouzwa zaidi katika soko la magendo na kwa dhulma ulimwenguni. Ukoo waliozaliwa ndani yake ina maana watashushwa hadhi na kudalalishwa chini ya hata mbwa - watumiwe vibaya mno, wauzwe kwa ukahaba na wadhulumiwe.



Ni hapa rafiki yangu Ryana alikutana na Landana, msichana mrembo sana akiwa na miaka kumi. Baba yake alikua na maafikiano kumuuza katika jumba la ukahaba India. Mama yake angeweza kusitiri wazo hilo la kumuuza na alijaribu kumzuia bwanake kumuuzu mwanawe mpendwa. Lakini bwanake hengesikia hilo. Alianza kumpiga bibi yake kwa sababu hakutaka wamuuzie msichana wao.



Walipo fahamu haya, walichukua hatua kwa haraka na kuwajulisha askari polisi na wafanyikazi wa serikali kijijini. Walimchukua Landana na kumpeleka katika nyumba yenye usalama ambapo wasichana kama yeye wanawekwa salama, wanalishwa na kupendwa. Landana akalisikia neno la Mungu. Akasikia vile kumpitia Yesu tumeasiliwa katita familia ya Mungu. Hii ndio sehemu ya injili yenye nguvu zaidi kwa wengi wanaoishi katika sehemu hii ya ulimwengu.



Ulipokuwa anashirikiana na msichana mwengine kutoka ukoo wa Badi, rafiki yangu Ryana alimwambia, "Injili inakufunza jina lako la mwisho halitakua tena Badi. Ni kama jina lako si tena Jaria Badi; ni Jarla 'Kristo' kwa sababu upo ndani ya familia yake, umeasiliwa katika ukoo wake sasa." Msichana huyo aliweza kunawiri na kumuangalia Ryan kwa macho ya uwezekano na matumaini. "Inaweza kuwa kweli?" akauliza. "Ndio, ndio ukweli wa kweli katika ulimwengu mzima!"



Landana kwa furaha alijiunga na familia ya Mungu, akiacha nyuma aibu ya familia yake, ukoo wake, tabaka lake. Mungu akawa babake, na upendo wake ni tofauti ya baba anayetaka kumuuza msichana wake kwa ukahaba. Ni Mungu aliyekuwa radhi kujiuza kwa vipande salasini vya fedha ili kumuoka msichana kama Landana.



Akili ya kisasa inauangalia ukristo na kustaajabu, "Kwa nini damu? Unaweza imba na kusifu vipi kuhusu damu ya Yesu?" Lakini kwa wale walionunuliwa kwa damu ya Yesu Kristo wanafahamu ya kwamba tuna ushirikiano unaotushikanisha pamoja kupita ukoo wetu hapa duniani. Yesu anatualika katika familia mpya na majaliwa mapya. Hii ndio sababu wakristo wanapenda kufikiria kuhusu damu ya Yesu Kristo.



Injili hii inazidi kutusamehe tu dhambi zetu za kale; inatusamehe makosa yetu ya ukoo, tabaka na aibu ziliko katika jamii zetu. Wewe si tu mmoja wa familia iliyopo hapa duniani tena; umejiunga na familia iliyo mbinguni. Damu ya Yesu imekuweka alama ya kukuingiza katika familia ya maisha ya milele. Tuna kitambulisho kipya katika jamii hii, ukoo mpya, uridhi mpya, mandungu na madada wapya, na jila la mwisho jipya.


siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Chosen: Remind Yourself Of The Gospel Everyday

Kutatokea nini kama utaamka kila siku na kijikumbusha juu ya injili? Masomo haya ya siku 7 yanalenga kukukumbusha hilo! Injili si kwamba inatuokoa tuu, bali hutuimarisha pia katika maisha yetu yote. Mwandishi na Mwinjili...

More

Tungependa kuwashukuru Think Eternity kwa kuwezesha mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tembelea tuvuti: https://www.thinke.org

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha