Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Waliochaguliwa: Jikumbushe Kuhusu Injili Kila SikuMfano

Chosen: Remind Yourself Of The Gospel Everyday

SIKU 1 YA 7

Kutatokea nini kama utaamka kila siku na kujikumbusha injili? 



Ukiwa kama mimi, unajaribiwa kuichukulia injili kirahisi tuu na kuacha kujizoeza kwa maana imezoeleka. Tunaitunza kwenye historia na katika fahamu zetu na kujaribu kuishi kwa mazoea. Lakini tunahitaji kusikia injili kila siku zaidi sana leo kama tulivyoisikia kwa mara ya kwanza. 



Kama tukijikumbusha injili kila asubuhi, tutaamka na kuishi katika furaha ambayo hata katika vita kali tutakayokabiliana nayo leo itakuwa tayari ushindi umepatikana. 



Maisha yako yatakuwa ni ya tofauti kiasi gani kama utahubiri injili kwa moyo wako mara kwa mara?



Kuna njia nyingi ambazo injili inabadilisha maisha yetu kila siku. Sisi sote tunahitaji kukumbushwa kila siku juu ya hizi faida, na tunahitaji nguvu za Mungu kuzifahamu zaidi. 



Waamini wengi wanadhani habari njema ni habari za zamani. Hatujasikia injili sana, hatujaisikia kwa wingi. Kama sura nyingi umbo la almasi, injili ina uzuri ambao hauwezi kuisha. Kwa kadri tunavyoiangalia injili, ndivyo tunavyopata nguvu na utoshelevu katika imani yetu.



Tunahitaji kujikumbusha yale yote ambayo Mungu ametufanyia katika injili, kwa sababu injili inatuchochea na kuhamasisha shauku ya kumtii Mungu na kumtumikia. Tunapoona jinsi alivyotufanyia, jinsi alivyotupa mwanaye-hatuna cha kufanya zaidi ya kumpa maisha yetu yote. Hata kama tu dhaifu na wenye dhambi tunaojitahidi kumfuata Yesu, injili inatukumbusha jinsi tunavyopendwa na jinsi Mungu anavyofanya kazi ndani yetu ili tumfuate. 



Hakuna hitaji kubwa katika maisha yako ya kikristo kuliko kujikumbusha mara kwa mara moyoni mwako juu ya ukweli wa injili. 


siku 2

Kuhusu Mpango huu

Chosen: Remind Yourself Of The Gospel Everyday

Kutatokea nini kama utaamka kila siku na kijikumbusha juu ya injili? Masomo haya ya siku 7 yanalenga kukukumbusha hilo! Injili si kwamba inatuokoa tuu, bali hutuimarisha pia katika maisha yetu yote. Mwandishi na Mwinjili...

More

Tungependa kuwashukuru Think Eternity kwa kuwezesha mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tembelea tuvuti: https://www.thinke.org

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha