Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Waliochaguliwa: Jikumbushe Kuhusu Injili Kila SikuMfano

Chosen: Remind Yourself Of The Gospel Everyday

SIKU 5 YA 7

Nilikuwa karibu kukiangusha chini kitabu cha David Bentley Hart nilipoona tafsiri yake ya neno "Aliyebarikiwa" katika Biblia. Msomi huyu maarufu anaongea kuhusu vile kubarikiwa kumepoteza maana katika tamaduni: inatumika kama "kuwa na bahati" ama "kufanikiwa". Badala yake, mwandishi Hart anatueleza maana ya kweli ya kubarikiwa inakaribia neno furaha ama hali ya kuwa na raha tele.



Hiki ndicho kitendo Mungu ametufanyia katika injili: Ametupatia kila baraka ya milele tunayowazia hadi tumefika mwahali pa kujaa furaha kabisa!



Maamuzi yetu ya kila siku, mapigano yetu ya kila siku, majaribu yetu ya kila siku si kana kwamba tutakumbuka, tutafahamu, ama tutaishi katika ukweli huu.



Na haitegemei hali zetu. Kwa kweli haitegemei hio. Kijana mdogo, kwa jina Meisha alinifunza hivi kwa njia ambayo sitasahau.



Meisha alikuwa mkimbizi katika nchi iliyokuwa na mapigano ya vita. Kijiji chake na yote yale aliyofahamu yaliharibiwa na jeshi lenye dhuluma, na alilazimishwa kuwa mbebaji, akibeba zana za wanajeshi kupita msitu mnene wakati wa mvua akiwa ameshikiwa bunduki usoni. - kama vile siku za Yesu wakati askari Mroma alipo mlazimisha mtu aubebe mzigo wake kwa maili.



Alafu siku moja askari jeshi alimlazimisha Meisha akiwa amemshikia bunduki atowanishe bomu ardhini. Bomu hilo lilirepuka, na Meisha akapoteza mikono yote na macho yote papo hapo. Wakamuacha pale, wakidhania amekufa, lakini alikua hai.



Miaka kadhaa baadaye, mtu alishiriki naye hadithi ya mkombozi aliyeteswa. Akajitambua na Mungu anaye elewa uchungu wake. Maisha yake yakabadilishwa kwa utakatifu.



Furaha ya Meisha inaambukiza. Ana furaha zaidi ya watu wengi wanao ona, wana mikono yote miwili, na hawaishi katika umaskini kama wale walioko katika kambi ya wakimbizi. Furaha yake inatokana na shukurani yake kwa sababu ya msalaba. Meisha anajua katika wakati mchache atakua na Yesu Kristo milele.



Meisha anauishi mfano huu kwa kushiriki neno la Mungu akiwa na furaha kubwa katikati mwa kambi hiyo ya wakimbizi. Meisha ni mfano bora wa maandiko ya Paulo, anayesema, "Taabu tunayopata ni kidogo, tena ya muda tu, lakini itakupatia utukufu upitao matazamio yote, utukufu ambao hauna mwisho. ( 2 Wakorintho 4:17).


siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Chosen: Remind Yourself Of The Gospel Everyday

Kutatokea nini kama utaamka kila siku na kijikumbusha juu ya injili? Masomo haya ya siku 7 yanalenga kukukumbusha hilo! Injili si kwamba inatuokoa tuu, bali hutuimarisha pia katika maisha yetu yote. Mwandishi na Mwinjili...

More

Tungependa kuwashukuru Think Eternity kwa kuwezesha mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tembelea tuvuti: https://www.thinke.org

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha