Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Waliochaguliwa: Jikumbushe Kuhusu Injili Kila SikuMfano

Chosen: Remind Yourself Of The Gospel Everyday

SIKU 2 YA 7

Rafiki yangu Ryan anasimulia hadithi kumhusu mtu anaye fahamika kama Mr. Bi aliyekuwa mhariri katika chuo kikuu cha Beijing, kinachofahamika kama "Havard ya China." Alifanya utani darasani kuhusu chama cha ukomunisti kwa kikundi cha wanafunzi. Mmoja ya wanafunzi hao akapiga ripoti kuhusu utani huo kwa polisi. Siku iliyofuata askari wa polisi waliingia kwa vishindo katika ofisi ya Mr. Bi na kumpeleka katika gereza lililoko mahali mbali, mwahali kwenye baridi - bila kumuonya wala kumshtaki mahakami.



Aliamka asubuhi hiyo kama mwalimu anayesimamia chuo chenye wasifu mkuu ulimwenguni. Usiku uliofwata, alikua gerezani. Magezera katika nchi ya Uchina wakati huo yalikuwa moja ya magereza yaliyokuwa katika hali mbaya zaidi ulimwenguni - kulikuwa magonjwa, kuteswa na mwishowe kifo. Mr. Bi alijipata amesononeka na kukosa matumaini. Kusononeka kwake kulielekea mawazo ya kujitoa uhai kwa wiki zilizofuatia. Alasiri moja, katika wingu la huzuni, alitembea hadi karibu na dirisha katika chumba chake cha futi nane gerezani. Wachina hawakuweka madirisha katika vyumba vya juu vya gorofa gerezani. Kama mfungwa aliamua kujirusha nje ya madirisha hayo haikua shida.



Moyo wa Mr. Bi ulipiga kwa kasi alipo angalia chini na kufikiria kujirusha. Alafu ikafanyika. Akasikia sauti ndogo, "Usiende. Usiende. Usiende." Alikaa chini katikati mwa chumba chake, bila matumaini.



Pale katika sakafu ngumu, kumbukumbu ilimjia. Rafiki yake, mwalimu kutoka ng'ambo aliyekuwa mkristo, alikuwa amemsimulia habari njema ya Yesu kristo. Mr. Bi aliomba, " Yesu, kama wewe ni Kweli, tafadhali nipatie msamaha na amani ambayo rafiki yangu alinieleze kwamba wewe Uliahidi. Nami nitayatoa maisha yangu kukutumikia wewe."



Alitizama juu na, " Mbingu haikubadilika, jua halikungaa zaidi ya kawaida dirishani mwake, na nilikua na furaha kupita kiasi katika moyo wangu kwa mara ya kwanza."



Huyu mwalimu mkuu aliacha ukuu wake na kuongea kwa sauti kuu, "Nina maisha bora sasa zaidi ya mbeleni katika Yesu Kristo!" Walinzi wa gereza walisikia hayo na kumuamuru anyamaze. Lakini furaha yake kuu haingeweza kunyamazishwa. Aliziki kuongea kwa sauti ya juu kwa mara zaidi ya moja mpaka walipokuja katika chumba chake na kumpiga.



Mtu gerezani aliwekwa huru kwa kuiamini injili ya Yesu ana uhuru zaidi ya mtu nje ya gereza asiye ifahamu injili.



Mr. Bi mwishowe aliachiliwa na kuanzisha nyumba za mayatima katika China bara, akiwajali mayatima na kuwaongoza wengi kwa Kristo. Ana maisha bora yenye mwelekeo katika Yesu Kristo. Hadi siku hii, raha yake inakuambukiza mkikutana naye. Na atakueleza furaha aliyonayo sana ni sawa na ile aliyekuwa nayo gerezani.



Kila mtu anahisi mara nyengine yupo katika gereza la kujitengenezea - kushikwa katika mawazo, tabia, vitendo, na maisha ya kale yanayo kuandama bila kukuachilia.



Injili inatufundisha kwamba gereza mbaya zaidi ni ile tunajitengenezea sisi wenyewe. Vyumba vya jela hii vina ushikilio wa kutojiamini, na uhakika kwambo kuna jambo lisilo sawa ndani yetu, kwamba ndani yetu kuna kitu kimevunjika. Tunabeba jambo hili kama nyororo shingoni mwetu. Ndio hali ya ubinadamu.



Hali hii itabadilika tu kama jambo kuu litafanyika.



Injili ndio jambo hili kuu. Ni msalaba ulio na damu. Ni kifo cha Mungu mwenyewe kwa ajili ya dhambi zetu. Ni ushindi wa kifo katika kufufuka ili kuonyesha mapenzi na nguvu za Mungu hadi katika uzima wa milele.



Neno linatukumbusha tutilie mkazo yale tuliyosikia, hasa sana inapokuja kwa Injili ( Waebrania 2:1). Mahubiri ya muhimu zaidi utakayo hubiri ni yale utakayo jihubiria moyoni mwako, kila siku ukijikumbusha, " Nina maisha bora zaidi mbeleni mwangu katika Yesu Kristo."


Andiko

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Chosen: Remind Yourself Of The Gospel Everyday

Kutatokea nini kama utaamka kila siku na kijikumbusha juu ya injili? Masomo haya ya siku 7 yanalenga kukukumbusha hilo! Injili si kwamba inatuokoa tuu, bali hutuimarisha pia katika maisha yetu yote. Mwandishi na Mwinjili...

More

Tungependa kuwashukuru Think Eternity kwa kuwezesha mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tembelea tuvuti: https://www.thinke.org

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha