Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Waliochaguliwa: Jikumbushe Kuhusu Injili Kila SikuMfano

Chosen: Remind Yourself Of The Gospel Everyday

SIKU 3 YA 7

Njia moja ya msingi tunayoifunza nafsi yetu kumpenda Mungu ni kuiubiria injili. Zaidi nafsi zetu zinauona msalaba wa Yesu, zaidi shukrani na ibada itakua ndani yetu. Wanadamu wameumbwa kujibu hivyo kwa kujitolea. Na ni ngumu kufikiria kujitolea zaidi ya vile Yesu alivyofanya.



Ukisafiri ulimwengui, kirai moja inayofana ulimwengu mzima - katika kila tamaduni - ni laini ya kwanza kutoka Zaburi 103:1 " Msifu Mwenyezi-Mungu, Ewe nafsi yangu."



Ifafanue kirai hii zaidi. Daudi anaifunza nafsi yake kwa kuiubiria. Daudi aliiambia nafsi yake jinsi ya kuhisi na kuijibu injili: Nafsi, msifu Mungu, ukipenda ama usipopenda. Akua tuu akiimba laini nzuri; alikua anajiongelesha, akiipa changamoto nafsi yake kujitolea zaidi. Neno linafafanua tabia hii, ikisema, " Daudi alijipa moyo katika Bwana (I Samueli 30:6, Bhn).



Nidhamu nzuri - ni kwa kweli sanaa uliyopotea katika Ukristo wa leo. Badala ya kutegemea unavyo hisi, utamaduni usio na nguvu, watu walio karibu nawe, ama, kwa hatari kuu, kutoka mitandao ya kijamii, itazame nafsi yako machoni na uiambie iangalie msalaba, kwa ufufuko. Iamuru nafsi yako kunywa ukarimu wa Kristo, aliye jeruhiwa na kuubeba mzigo wa dhambi katika mabega yake.



Wakati mwengine inabidi kuilazimu nafsi yako kuangalia. Yohana Mbatizaji aliuita ulimwengu, "Angalia!" ama " Lazima uangalie!" Akasema, " Tizama, Mwanakondoo wa Mungu, aondoae dhambi za ulimwengu!" (Yohane 1:29, Bhn). Hii ni amri ya kila siku. Lazima tutazame! Utazamie msalaba ambapo Yesu aliteseka sana kwa dhambi ambayo hakufanya ili uweze kufurahia katika utakatifu ambao hukustahili.



Injili inakua chakula cha kila siku kwa nafsi zetu, kuipatia nguvu mioyo yetu. Ni vigumu kulalama, kujionea huruma, ama kuwa na shauku wakati nafsi zetu zinaona damu ikitiririka chini ya uso wa Yesu uliovalishwa taji la mwiba. Shukrani inaijaa mioyo yetu tunapofanya hivi muda wote katika siku zetu.


siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Chosen: Remind Yourself Of The Gospel Everyday

Kutatokea nini kama utaamka kila siku na kijikumbusha juu ya injili? Masomo haya ya siku 7 yanalenga kukukumbusha hilo! Injili si kwamba inatuokoa tuu, bali hutuimarisha pia katika maisha yetu yote. Mwandishi na Mwinjili...

More

Tungependa kuwashukuru Think Eternity kwa kuwezesha mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tembelea tuvuti: https://www.thinke.org

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha