Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Oswald Chambers: Furaha- Nguvu katika BwanaMfano

Oswald Chambers: Joy - Strength In The Lord

SIKU 1 YA 30

Furaha inamaanisha kutimizika kikamilifu kwa nia ya uumbaji wangu na kufanywa upya, si kufanikiwa katika jambo. Furaha ya Bwana wetu ilikuwa katika kufanya yote ambayo Baba alimtuma kufanya. Ni lazima tupate nafasi yetu katika maisha na kiroho tunaipata tunapopokea huduma yetu kutoka Mungu. Ili kufanya hivi lazima tuwe marafiki na Yesu; lazima tumjue zaidi ya kuwa mwokozi wangu pekee. Nimepokea huduma kutoka Bwana? Ikiwa nimepokea, lazima niwe mwaminifu, kukiri kwamba maisha yangu ni yenye thamani kwa sababu ni lazima huduma hiyo itimizwe.



Bwana, naja kwako. Nijaze furifuri na maisha yako mpaka hoja zangu, mawazo yangu, na maneno yangu ni kuhusu wewe. Ninashangaa jinsi umeweka ndani yangu roho mpya na umenirudishia furaha ya wokovu wako!



Maswali ya Kutafakari: Nafasi yangu kiroho ni wapi? Ni nini ninafanya ambacho ni mimi pekee ninaweza kufanya? Huduma yangu kutoka Bwana ni nini? Je, mimi ni mwaminifu? Kwa njia gani maisha yangu ni yenye thamani kwa Yesu?



Dondoo zimetoka "Called of God" na "Knocking at God’s Door", © Discovery House Publishers

Andiko

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Oswald Chambers: Joy - Strength In The Lord

Gundua hekima ya Oswald Chambers, mwandishi wa "My Utmost for His Highest", katika mkusanyiko huu wa hazina ambao unatoa ufahamu kuhusu furaha. Kila somo lina dondoo kutoka Chambers na maswali ya kutafakari kibinafsi. Ak...

More

We would like to thank Discovery House Publishers for providing this plan. For more information, please visit: www.utmost.org

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha