Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Oswald Chambers: Furaha- Nguvu katika BwanaMfano

Oswald Chambers: Joy - Strength In The Lord

SIKU 8 YA 30

Nia kuu ya utumishi si kwamba Mungu ameniokoa na kunitakasa ama ameniponya. Yote hayo ni kweli, lakini nia kuu ya utumishi ni ugunduzi kwamba ninadai Ukombozi kila sehemu ya maisha yangu iliyo na thamani. Ninagundua kwa furaha kwamba siwezi kuishi maisha yangu mwenyewe; mimi ni mdaiwa wa Kristo, kwa hivyo nitashuhudia kutimizika kwa madhumuni yake pekee maishani mwangu.



Furaha ya Yesu Kristo ilikuwa kujisalimisha amri na kujitolea kikamilifu kwa Baba yake, furaha ya kufanya yale ambayo Baba alimtuma kufanya, na hiyo ndiyo furaha anayoombea wafuasi wake waweze kushiriki. Si suala la kujaribu kufanya kazi kama Yesu alivyofanya, bali kuwa na uwepo binafsi wa Roho Mtakatifu anayefanya ndani yetu Ukristo. Faraja mojawapo ni jinsi furaha isiyoeleweka ya Roho Mtakatifu inadhihirika ndani yetu kama vile ilivyoonekana ndani ya Mwana wa Mungu alipokuwa mwanadamu.



Maswali ya Kutafakari: Ni nini inayofurahisha kugundua kwamba hatuwezi kuishi maisha yetu wenyewe? Ikiwa Yesu alipata furaha katika kujisalimisha, ni nini ninayoweza kutarajia kwa sababu Kristo anaishi kupitia kwangu?



Dondoo imetoka "So Send I You", © Discovery House Publishers
siku 7siku 9

Kuhusu Mpango huu

Oswald Chambers: Joy - Strength In The Lord

Gundua hekima ya Oswald Chambers, mwandishi wa "My Utmost for His Highest", katika mkusanyiko huu wa hazina ambao unatoa ufahamu kuhusu furaha. Kila somo lina dondoo kutoka Chambers na maswali ya kutafakari kibinafsi. Ak...

More

We would like to thank Discovery House Publishers for providing this plan. For more information, please visit: www.utmost.org

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha