Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Mambo 7 ambayo Biblia inasema kuhusu UzaziMfano

7 Things The Bible Says About Parenting

SIKU 7 YA 7


Miaka kadhaa iliyopita, tulipiga hatua na kuelekea ndani ya mwito wa Mungu ili kukuza familia yetu kupitia kuasili na kulea. Tulijua itakua ngumu, lakini tulikua tayari kua mikono na miguu ya Mungu kwa familia zetu wakati wanapotuhitaji. Tulikua tayari kubadilisha dunia mzima. Lakini lile hatukujua ni jinsi Mungu angebadilisha duniayetu.


Watu mara nyingi hutuambia jinsi sisi ni wa pekee kwa kufanya hivi. Lakini wacha nikuambie siri: wazazi wanaasili sio maalum. Tumevunjika; sisi hufanya makosa; tunapiga makelele, na hakuna shaka kwamba hatuko sawa kila wakati. Tunatembea kwa imani na kujirusha ndani ya fujo. Kile kilicho cha pekee, lakini, ni kile Mungu hufanya tunapomskiza na kumfuata.


Tumemuona Mungu akijitokeza mara kwa mara miaka kadhaa iliyopita kama familia asilia, akisongesha milima zaidi tunayokumbuka kuliko hapo awali. Tulipofikiria kwamba hakuna matumaini ya uhusiano na familia ya kibiolojia ya mtoto, Mungu alijitokeza. Wakati ulipofika wa kuambia watoto wengine tuliowalea kwaheri, Mungu alijitokeza. Tulipofikira kwamba hatutaweza kumaliza siku nyingine, Mungu alijitokeza.


Safari hii imetusaidia kumwelewa jinsi Mungu anatutazama. Kama tunavyo waalika wototo wanaoumia ndani ya nyumba yetu, Mungu ametualika ndani ya familia yake. Yeye ni Baba Wetu Aliye Mbinguni na mlinzi wetu. Hajali kuhusu shida zetu, dhambi tulizofanya, ama jinsi tusivyojiweza. Tukielekea Kwake, Anatukumbatia kama baba, anatupenda bila masharti, na anatuita kama ndugu na dada Zake.


Kama unahisi huwezijimudu, kama unahisi unapitia changamoto zaidi ya uwezo wako, ama hujui kile utakachofanya, nakusihi umtafute Mungu na ujirushe ndani mwake. Watu wanaweza kufikiria umerukwa na akili. Kwa kweli, najua watafikiria hivyo. Lakini naweza kukuhakikishia hili: Mungu tayari anakutafuta. Na Akona mpango wa maisha yako uliozidi fikra zako leo.


Taylor Ketron
Msimamizi wa YouVersion


Andiko

siku 6

Kuhusu Mpango huu

7 Things The Bible Says About Parenting

Kulea watoto ni kazi kubwa, hata katika mazingira bora. Katika mpango huu wa ibada wa siku saba, wazazi wa ulimwengu halisi -ambao pia wametokea kuwa wafanyakazi wa YouVersion - wanatushirikisha jinsi wanavyotumia kanuni...

More

Tungependa Kushukuru YouVersion kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya http://www.bible.com/reading-plans

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha