Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Mambo 7 ambayo Biblia inasema kuhusu UzaziMfano

7 Things The Bible Says About Parenting

SIKU 6 YA 7


Nilikua na maumivu ya kujifungua kwa saa 60. Saa 60 ndefu, zilizojazwa na wasiwsi na za kuumiza. Wanawake wengine walilalamika ju ya muda huo mrefu, huku wengine wakijivunia kwamba waliweza kuvumulia uchungu huo kwa muda mrefu. Ningesema kwamba mimi najiunga na kikundi kinachojivunia kuvumulia muda huo mrefu wa kuchosha.


Lakini kiburi hiyo ilififia mvulana wangu alipoanza kulia usiku wa manane, saa chache baada ya kuzaliwa kwake. "Mlio huu unamaanisha nini? Anahisi njaa? Atakula kiasi gani? Anahitaji kitu kingine?
Muuguzi yuko wapi?!?"


Kuzaliwa kwa mvulana wangu ulinipa shukrani mkubwa kwa zawadi ya maisha. Lakini, nyuma ya shukrani huo mkubwa, hisia za shaka, woga na kutojiweza zilifuata. Kama mama mara ya kwanza, nilijihisi kwamba sikua nimejitayarisha vilivyo kumenyana na uzazi.


Ukweli usemwe, hisia hizo bado jazijapotea. Lakini naamini Biblia inaposema:


Ukihitaji busara mwulize Mungu wetu aliye mkarimu, na Atakupea.
Yakobo 1:5


Mungu alinionyesha kiwango kipya cha ukarimu wake kwa kunipa zawadi ya mtoto, na upya wa msimu huu uliniweka pahali pa kumwulizia Mungu anipe busara kwa unyenyekevu. Amekua mwaminifu kwa kuelekeza uzazi wangu na ukarimu wake wakati wowote ninapoenda kwake na nafsi ya kujisalimisha na usikivu.


Natarajia kwamba unajua rasilimali uliyonayo kupitia Yesu Kristo. Anataka kuendelea kumwaga ukarimu wake juu yako kupitia njia unavyolea wattot wako. Anataka-kukushinda-mtoto wako amjue, ampende, amtumikie na amwelekeze. Yeye ana busara na ni mkarimu, na ako tayari kukumwagia yote mawili kwa wingi mno. Uko tayari kuyakumbatia?


Enda kwa Mungu wetu mkarimu na umwulize akupe busara unapopitia changamoto za uzazi. Ako tayari kukupea hekima.


Jessica Penick


Meneja wa Yaliyomo YouVersion


Andiko

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

7 Things The Bible Says About Parenting

Kulea watoto ni kazi kubwa, hata katika mazingira bora. Katika mpango huu wa ibada wa siku saba, wazazi wa ulimwengu halisi -ambao pia wametokea kuwa wafanyakazi wa YouVersion - wanatushirikisha jinsi wanavyotumia kanuni...

More

Tungependa Kushukuru YouVersion kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya http://www.bible.com/reading-plans

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha