Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Mambo 7 ambayo Biblia inasema kuhusu UzaziMfano

7 Things The Bible Says About Parenting

SIKU 2 YA 7


Ilikuwa Juni 2010, mke wangu na mimi tulikuwa karibu tunapata mtoto wetu wa kwanza. Tulikuwa tunakula chakula cha jioni na baba yangu, kwa hiyo nikaamua kuomba hekima kidogo. Nikamuomba baba anipe ushauri bora aliokuwa nao kwa miaka mingi kuhusu malezi.


Alifikiria kwa muda, kisha akanipa maelezo ambayo sitasahau. Baba alisema malezi ni kama mzani, -si kama unaojipimia bafuni, lakini kama ule unaouona kwenye alama ya haki. Upande mmoja una upendo; upande mwingine una nidhamu. Kutumia upande mmoja mara nyingi bila mwingine ina madhara kwa mtoto.


Baba aliendelea kuelezea kwamba kwa kadri unavyoonesha upendo kwa mtoto, ndivyo kadri watakavyopokea kuadabishwa. Na, utakapotumia nidhamu zaidi kwao, unatakiwa pia uwaonesha unawapenda kiasi gani. Kuwapenda zaidi bila nidhamu lkunaweza kuwaathiri watoto, na adhabu ikizidi bila upendo inaweza kuharibu hisia za mtoto na kumkimbiza.


Tangu usiku ule, siku zote nafikiria uhusiano wa maonyo na upendo. Naamini wazazi mara nyingi hujisikia vibaya wanapowaadhibu watoto wao. Hakika si jambo la mzaha kuadhibu. Ni ngumu, lakini ni vizuri. Kwa hiyo ushauri wangu kwako ni kutumia viwango sa hihi vya adhabu kwa watoto wako ili kwamba wajue unawapenda na kuwajali.


Kama tunavyowapenda watoto wetu na kutaka kuwaadabisha, baba yetu wa mbunguni anawapenda watoto wake na atawaadabisha. Kama umempokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wako, kwa hiyo Mungu ni baba yako. Umeasiliwa katika familia yake.


Brad Belyeu
YouVersion Engineer 


Andiko

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

7 Things The Bible Says About Parenting

Kulea watoto ni kazi kubwa, hata katika mazingira bora. Katika mpango huu wa ibada wa siku saba, wazazi wa ulimwengu halisi -ambao pia wametokea kuwa wafanyakazi wa YouVersion - wanatushirikisha jinsi wanavyotumia kanuni...

More

Tungependa Kushukuru YouVersion kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya http://www.bible.com/reading-plans

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha