Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Kubaki Katika KristoMfano

Kubaki Katika Kristo

SIKU 5 YA 5

Ibada ya Siku ya Tano

Umalizio

Wakati wa Vita vya Pili vya Ulimwengu, kundi moja la jeshi la Uingereza lilikamatwa na kuwekwa gerezani na Jeshi la Japani. Mwishoni mwa siku ya kazi ngumu, wale askari walikagua na kuhesabu zile sepetu walizotumia kwa kazi wale wafungwa wakiingereza katika kambi ya gereza na wakapata sepetu moja ilikosekana.

Kwa hasira kuu, askari mmoja wa Kijapani aliwatisha wale wafungwa wa vita kwamba lazima aliyekuwa na hatia ya kile kitendo akiri la sivyo angewauwa wafungwa wote. Alitayarisha bunduki yake ili kuanza kuwapiga risasi mmoja baada ya mwingine. Wakati huo huo, mmoja wa wale wafungwa wa Kiingereza alisonga mbele na kwa taratibu akasema, “ni mimi nilifanya hivyo.”

Yule mwanajeshi wa Kiingereza alisimama kimya huku akipigwa na wale wanajeshi wa Kijapani mpaka akafa. Basi wale wanajeshi wa Kiingereza waliporudi katika Kambi, walihesabu zile sepetu tena, na waligundua kuwa zote zilikuwepo pale. Yule mwanajeshi mmoja alijitoa sadaka ili kuwaokoa wenzake.

Sadaka ya huyo mwanajeshi inatukumbusha vile Kristo anatuambia katika Yohana 15:13: Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhaiwake kwa ajili ya rafiki zake.

Acheni niwaonyeshe tofauti kubwa zaidi kati ya kitendo cha yule mwanajeshi wa Kiingereza na kile alichokitenda Kristo. Unaona, yule mwanajeshi wa Kiingereza alikufa kwa niaba ya wenzake ambao walikuwa marafiki zake. Lakini Kristo, alitoa uhai wake kwa ajili yetu, sisi ambao katukuwa marafiki zake, bali maadui zake.

Tulikuwa maadui zake kwa sababu kiasili sisi ni wanadhambi walioasi Mungu, kitendo ambacho kilitugeuza kuwa adui wa Mungu, na bado Kristo alijitoa uhai kwa ajili yetu, adui zake!

Warumi 5:8 inatukumbusha hili na kutuambia kwamba, tulipokuwa tungali wenye dhambi, Kristo alikufa kwa ajili yetu. Hii ni Habari njema kuu kuhusu injili ya Yesu Kristo.

Injili inatukumbusha kwamba, kwa sababu Kristo aliteseka kwa uchungu mwingi, ukosefu wa haki, na kifo cha kikatili kwa niaba yetu sisi ambao tunaokistahili kifo hicho, ni muhimu kumwamini na kubaki ndani yake.

Kristo alitumia neno Kubaki au Kukaa mara kumi katika kifungu hiki. Hii inasisitiza dharura ya kubaki ndani yake ili Roho Mtakatifu aendelee kutujaza furaha ya Kristo tunapokutana na uchungu wa mapito ya kupogolewa ambayo Kristo ataruhusu katika maisha yetu ya Ukristo.

Bwana anavyotuongoza mahali pagumu ambapo barabara za maisha yetu ya Ukristo, hebu somo hili kutokana na Mpango huu ututie moyo sote, kupitia Roho Mtakatifu, ili tubaki ndani ya Kristo, na kuweza kuzaa matunda mengi ya ndani na nnje ya Kiroho.

siku 4

Kuhusu Mpango huu

Kubaki Katika Kristo

Katika kifungu hiki, kwanza, Kristo anatuwezesha kuelewa maana ya kubaki ndani yake. Pili, Kristo anatuwezesha kuelewa taratibu zinazochangia kuimarisha kubaki au kukaa ndani yake. Tatu, Kristo, anafafanua alama tatu zin...

More

Tungependa kuwashukuru Emmanuel Kwasi Amoafo kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://returningtothegospel.com/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha