Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Kubaki Katika KristoMfano

Kubaki Katika Kristo

SIKU 4 YA 5

Ibada ya Siku ya Nne

Alama Zinazotutambulisha Tumo Ndani ya Kristo

Katika kifungu hiki, Kristo pia anafafanua njia tatu ambazo ukristo wetu unaonyesha dhahiri kuwa tunadumu ndani yake.

Njia ya kwanza ambayo inaonyesha alama maalum kuwa tumo ndani ya Kristo ni kwamba tunaendelea kuzaa tunda la Roho Mtakatifu ndani na nnje. Mara saba katika kifungu hiki Kristo anarejelea jambo hili la kuzaa matunda.

Wagalatia 5:22 inazungumzia na kufafanua juu ya mazao ya Roho au tunda la Roho kuwa upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi au kujitawala. Hizi ndizo tabia za Kristo mwenyewe na zinazaliwa maishani mwetu tunavyojifunza kila siku tunaponyenyekea chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu ambaye baada ya uokovu wetu anatupa uhai wa kristo. Hapo basi tunazaa matunda ya nnje ili watu waone na kuonja tunda lililopo ndani maishani mwetu, na kuvutiwa na Kristo aliye ndani yetu kwani ni uhai wake tunaouonyesha.

Njia ya pili katika Maisha yetu inayoonyesha tumebaki ndani ya Kristo inapatikana mstari wa 11 ambapo Kristo anatuambia kwamba tukibaki ndani yake, furaha yake itadumu ndani yetu. Katika Agano Jipya, neno hili furaha linamaanisha kuwa katika utulivu na ujasiri mbele ya ugumu wa maisha. Kubaki ndani ya Krist, inamaanisha, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, tunaweza kuendelea kukutana na changa moto za maisha kwa uwezo na mwongozo wa Roho Mtakatifu.

Njia ya tatu ambayo maisha ya Mkristo yana alama ya kudumu ndani ya Kristo inapatikana mstari wa 7 na 16. Hapa Kristo anatuahidi kwamba tukibaki ndani yake, na kutii neno lake, sala zetu zitasikika na kujibiwa. Tunapobaki ndani ya Kristo tunajenga uhusiano wetu naye, na kuomba zaidi na zaidi kulingana na mapenzi yake, na kwa kufanya hivyo, tunapata majibu ya maombi yetu. (1 Yohana 5:14-15)

Kwa kifupi, tunasema kwamba njia tatu zinazodhihirisha kuwa tumo ndani ya Kristo ni , Kwanza, kuzaa tunda la kiroho, pili, kujionea furaha ya Bwana, na tatu, kupokea majibu kwa maombi yetu.

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Kubaki Katika Kristo

Katika kifungu hiki, kwanza, Kristo anatuwezesha kuelewa maana ya kubaki ndani yake. Pili, Kristo anatuwezesha kuelewa taratibu zinazochangia kuimarisha kubaki au kukaa ndani yake. Tatu, Kristo, anafafanua alama tatu zin...

More

Tungependa kuwashukuru Emmanuel Kwasi Amoafo kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://returningtothegospel.com/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha