Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Kubaki Katika KristoMfano

Kubaki Katika Kristo

SIKU 3 YA 5

Ibada ya Siku ya Tatu

Taratibu Zinazoimarisha Kubaki Ndani ya Kristo

Katika ukurasa huu, Kristo anatuonyesha taratibu tatu zinazoimarisha kubaki au kukaa ndani yake.

Taratibu ya kwanza inapatikana katika kifungu cha tatu ambapo Kristo anawaambia wanafunzi wake kwamba ni wasafi kwa sababu ya neno lake alilowapa. Katika vifungu vya 7, 10, 14, na 15, Kristo anasema kuwa maneno yake yabaki ndani yetu, nasi tulitii neno lake. Hivi vifungu vinatufunza kuwa taratibu ya kwanza inayotuimarisha katika Kristo ni kulitia maanani neno la Mungu tunavyoendelea kuamua kulitii hilo neno kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.

Taratibu ya pili inapatikana katika vifungu vifuatavyo: 10, 12, 13, na 17. Katika vifungu hivi, Kristo anaelezea kwamba taratibu ya pili inayoimarisha kubaki ndani yake kwa kimakusudi ni upendo kati yetu ambapo huo uamuzi wa kupendana unatuunganisha pamoja kama wafuasi wa Kristo. Asili ya neno upendo kwa Kigiriki anaoutumia Kristo katika vifungu hivi kwa uhalisi unamaanisha kujitahidi kupendana au kujizoeza upendo. Zoezi linamaanisha matendo, na sio hisia au matamko pekee.

Kwa hivyo, hapa Kristo anasema kwamba tunafaa kupendana kwa njia za matendo kama kuonyeshana fadhili, ukarimu, subira, upole, kusameheana, na kadhalika. Kristo alionyesha upendo wa aina hiyo kwetu sisi aliposulubishwa msalabani kwa ajili yetu (mstari wa 13).

Taratibu ya tatu inapatikana msitari wa 7 na 16. Hapa, Kristo anaeleza kwamba taratibu inayotuimarisha kudumu ndani yake ni kuwa na tabia kibinafsi imara ya sala. Sala ya kweli ni mazungumzo ambapo tunanena na tunamsikiza Bwana kwa sababu hatuwezi kuwa na uhusiano wa maana naye Bwana, au mtu yeyote, kama hatuzungumzi naye au kuwasikiza.

Kwa hivyo, taratibu hii ya tatu, inayohitaji tabia imara za sala za kibinafsi, itatuwezesha kuendelea na uhusiano na Mungu ulio hai na wa maana na kuimarisha kukaa ndani yake tunapoendelea kukua katika imani yetu na kumtii Bwana.

Basi , kwa ufupi tunaweza kusema kuwa taratibu tatu au nidhamu za kiroho zinazoimarisha Kubaki ndani ya Kristo ni kudumu katika neno la Mungu, kupendana, na kujitolea kukuza na kuzingatia tabia za kibinafsi za maombi au sala.

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Kubaki Katika Kristo

Katika kifungu hiki, kwanza, Kristo anatuwezesha kuelewa maana ya kubaki ndani yake. Pili, Kristo anatuwezesha kuelewa taratibu zinazochangia kuimarisha kubaki au kukaa ndani yake. Tatu, Kristo, anafafanua alama tatu zin...

More

Tungependa kuwashukuru Emmanuel Kwasi Amoafo kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://returningtothegospel.com/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha