Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022

SIKU 4 YA 31

Maana kwa sababu hiyo nilitumwa (m.43). Jambo kubwa kwa Yesu ni kuhubiri na kufundisha habari njema ya Ufalme wa Mungu kila mahali. Ndiyo maana alikuwa akifundisha katika masinagogi yao, Akawaambia, Imenipasa kuihubiri habari njema ya ufalme wa Mungu katika miji mingine pia; maana kwa sababu hiyo nalitumwa. Na alikuwa akihubiri katika masinagogi ya Galilaya (m.15, 21f, 43f). Katika Mk 1:15 kuna muhtasara wa alivyofundisha: Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili. Matendo ya upendo ambayo Yesu aliwatendea watu yalithibitisha mafundisho yake juu ya ufalme huo. 1. Yesu aliwasaidia watu bure. Hakudai chochote. Yaani watu hukaribishwa kuingia katika ufalme wake bure! Ndivyo alivyowaagiza wanafunzi wake wakifanya kazi ya Mungu: Hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia. Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure (Mt 10:7-8). 2. Yesu aliponya kila aina ya ugonjwa, alitoa mapepo yote na aliwafufua wafu. Yaani ufalme wake hauna maradhi wala maovu wala mauti! Ahadi ya Yesu ni kwamba atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita (Ufu 21:4; ukiwa na nafasi tafuta kusoma mistari yote ya 1-7).

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Oktoba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma k...

More

http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha