Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022

SIKU 9 YA 31

Wakiyapukusa-pukusa mikononi mwao (m.1). Maana yake ni kwamba waliondoa punje zake kwa mikono. Leo twajifunza kuwa tusifungwe na amri za kibinadamu bali na amri za Mungu tu. Amri moja ya Mungu inasema: Siku ya saba ni sabato ya Bwana, Mungu wako; siku hiyo usifanye kazi yo yote (Kum 5:14). Viongozi wa dini ya Kiyahudi walikuwa wametafakari sana amri hii na kutengeneza orodha ndefu ya kazi zisizokuwa za halali kufanya siku hiyo. Mafarisayo walishika sana hayo. Kwa hiyo wanawauliza wanafunzi wa Yesu, Mbona mnafanya lisilo halali siku ya sabato? (m.2). Lakini Yesu aliwakemea. Akawaambia, Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato (m.5). Nawauliza ninyi, Je! Ni halali siku ya sabato kutenda mema, au kutenda mabaya; kuponya roho au kuangamiza? Akawakazia macho wote pande zote, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Akaunyosha; mkono wake ukawa mzima tena (9-11). Sababu ya msingi ya Yesu kufanya hivyo ipo katika Mt 22:39-40 anaposema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.

Andiko

siku 8siku 10

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Oktoba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma k...

More

http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha