Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022

SIKU 2 YA 31

Siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake (m.16). Desturi nzuri zinatusaidia sana kutunza vizuri maisha yetu ya kiroho. Kwa mfano desturi ya kusali Jumapili au kushukuru kwa chakula au kuwa na maombi wakati wa kuamka na wakati wa kulala au kusoma Biblia kila siku n.k. Jitahidi uwe na desturi nzuri katika mambo haya. Jambo likiwa desturi utalikumbuka kwa urahisi na utalifanya kwa furaha. Yesu anasema, Utafuteni kwanza ufalme wake [Mungu], na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. Zingatia pia shauri la Kol 3:16-17, Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye. Watu wa nyumbani walimkataa Yesu kama Mwokozi wao. Akashindwa kuwasaidia. Basi akawaambia, Hapana shaka mtaniambia mithali hii, Tabibu, jiponye nafsi yako; mambo yote tuliyosikia kwamba yametendeka Kapernaumu, yatende na hapa pia katika nchi yako mwenyewe. Akasema, Amin, nawaambia ya kwamba, Hakuna nabii mwenye kukubaliwa katika nchi yake mwenyewe (m.23f).

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022

Soma Biblia Kila Siku Oktoba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Oktoba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma k...

More

http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha