Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Juni/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Juni/2022

SIKU 22 YA 30

Yuda alikuwa ametenda maovu. Alikuwa ameongoza mauzo ya ndugu yake Yusufu. Akawa hana raha!Akashuka kutoka kwa ndugu zake, akamfikia mtu Mwadulami, jina lake Hira(m.1). Afadhali kama angalienda kwa baba yake, lakini aliogopa kumwona! Sasa akazidi kujiingiza katika matatizo kwa kumwoa mkanaani, mtu asiyemcha Mungu (m.2). Ndipo wana wake nao wakawa watu wasiomcha Mungu! Wawili wakafa mapema kwa mkono wa Mungu kutokana na uovu wao (m.7 na 9-10)! Unapandaje? Jipime kwa kusoma Gal 6:7-10 usikie Neno linavyosema:Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele. Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho. Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.

siku 21siku 23

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Juni/2022

Soma Biblia Kila Siku Juni/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Juni pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa s...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha