Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Juni/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Juni/2022

SIKU 12 YA 30

Wakristo wote hatuishi kwa hasara wala hatutaishia hasara. Maana tumeitwa na Mungu tufikilie kwake mbinguni na kupewa kuishi naye milele. Hiyo ndiyo mede au taji yetu. Ni thawabu ya ushindi wetu. Ushindi huo humtegemea Yesu ambaye atatushika hata tufikie hayo. Kazi yetu ni kukaza mwendo mithili ya mkimbiaji ashindanaye kunyakua taji iliyoko mbele yake. Tusiogope kuipoteza, maana Yesu anatushika. Mtume Paulo anasema, Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu(mst.12). Hii ni sawa na sala ya Bwana Yesu aliyoiomba akisema,Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe(Yn 6:37). Kwa hiyo, tukimkazia Yesu macho yeye hali tukimtegemea, atatutia nguvu.

siku 11siku 13

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Juni/2022

Soma Biblia Kila Siku Juni/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Juni pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa s...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha