Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022

SIKU 3 YA 30

”Thenashara” (m.3), maana yake ni 12. Ni wale aliowachagua Yesu kipekee na kuwaita mitume. Hata hivyo mmoja wao (Yuda Iskariote) akaanguka na kuamua kumsaliti Yesu. Hili ni onyo hasa kwa viongozi wa kanisa:Anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke(1 Kor 10:12). Mungu alikuwa amepanga tayari mwisho wa maisha ya Yesu, hatua kwa hatua. Fikiria habari zifuatazo katika m.7-13: Yesuakawaambia, Tazama, mtakapoingia mjini mtakutana na mwanamume akichukua mtungi wa maji ... Na mtamwambia mwenye nyumba, Mwalimu akuambia, Ki wapi chumba cha wageni, nipate kula pasaka humo pamoja na wanafunzi wangu? Naye atawaonyesha chumba kikubwa orofani, kimekwisha andikwa ... Wakaenda, wakaona kama alivyowaambia. Kwa kawaida wanaume hawakubeba mtungi wa maji, kwa hiyo habari katika m.10 ya kuwamtakutana na mwanamume akichukua mtungi wa maji,ni ya ajabu. Kumbuka pia 18:31-33:Akawachukua wale Thenashara, akawaambia, Tazameni, tunapanda kwenda Yerusalemu, na mambo yote yatatimizwa, Mwana wa Adamu aliyoandikiwa na manabii. Kwa kuwa atatiwa mikononi mwa Mataifa, atafanyiwa dhihaka; atatendwa jeuri, na kutemewa mate; nao watampiga mijeledi, kisha watamwua; na siku ya tatu atafufuka. Ni wazi kwamba Yesu alijua mambo kabla hayajatokea, maana amejulishwa mpango huo.

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Aprili pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma k...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/

Mipangilio yanayo husiana

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha