Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022

SIKU 6 YA 30

Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki … katika dhiki akazidi sana kuomba; hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini(m.42, 44). Yesu ametangaza kifo chake mara tatu:1)Akisema, Imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi, na kukataliwa na wazee na wakuu wa makuhani na waandishi, na kuuawa na siku ya tatu kufufuka(9:22),2)Yashikeni maneno haya masikioni mwenu, kwa kuwa Mwana wa Adamu anakwenda kutiwa katika mikono ya watu(9:44), na3)Kwakuwa atatiwa mikononi mwa Mataifa, atafanyiwa dhihaka; atatendwa jeuri, na kutemewa mate; nao watampiga mijeledi, kisha watamwua(18:32-33).Hata hivyo si jambo rahisi kwa Mwokozi wetu mpendwa kwenda njia hii! Mbele yake kuna mateso makali kupita kiwango. Katika m.37 amesema itatimia kama ilivyoandikwa kuhusu yeye kwambaalihesabiwa pamoja na wahalifu. Kutendewa kama mhalifu hutisha. Ila mzigo mkubwa zaidi ni dhambi zetu.Atapigwa na Mungu, na kuteswabadala yetu ili sisi tupate kupona (Isa 53:4-6)! Je, umemshukuru?

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022

Soma Biblia Kila Siku Aprili/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Aprili pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma k...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/

Mipangilio yanayo husiana

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha