Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022

SIKU 7 YA 31

Hatujui kama Ibrahimu alimwoa Ketura kabla au baada ya kifo cha Sara. Kwa Ketura alipata wana sita zaidi. Hata hivyo ni kwa njia ya Isaka peke yake Mungu alitaka kutimiza ahadi yake ya kumpa Ibrahimu na uzao wake nchi ya Kanaani. Na Ibrahimu aliheshimu mpango huu wa Mungu. Ndiyo maana twasoma kwamba wale wana aliopata kwa Ketura aliwapa zawadi na kuwaondoa wasikae katika nchi ya Kanaani (m.6, Wana wa masuria aliokuwa nao Ibrahimu, Ibrahimu akawapa zawadi, naye akawaondoa katika mahali alipokaa Isaka mwanawe, wakati wa uhai wake). Ila Isaka alirithi mali yake yote, na Mungu akambariki (m.5 na 11, Ibrahimu akampa Isaka yote aliyokuwa nayo … Ikawa, baada ya kufa kwake Ibrahimu, Mungu akambariki Isaka mwanawe)! Imani yake ilizaa matendo!

siku 6siku 8

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha