Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022

SIKU 8 YA 31

Isaka alipomwoa Rebeka alikuwa na miaka 40. Lakini ikapita miaka 20 mpaka Rebeka akamzalia watoto, yaani, Esau na Yakobo (m.26, Isaka alikuwa mwenye miaka sitini mkewe alipowazaa). Hata hivyo Isaka akawa mwaminifu kwa mke wake miaka yote hii. Badala ya kumlaumu, akazidi kumpenda. Akamshirikisha Mungu tatizo la Rebeka: Isaka akamwomba Bwana kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa. Naye Bwana akamwitikia (m.21)! Je, msomaji, wewe ni mwaminifu kwa mwenzako na kumwombea kwa Mungu katika matatizo yake? Kuwa mwaminifu ni pamoja na kumpenda mwenzako na kumheshimu. Hivi ndivyo inavyompasa mkristo, yaani, ... kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mumewe (Efe 5:21-33).

siku 7siku 9

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha